Makubaliano ya amani yatiwa saini Yemen

Serikali ya Yemen imetiliana saini makubaliano ya amani na waasi wa kishia wa Houthi yaliosimamiwa na Umoja wa Mataifa. Makubaliano hayo yanalenga kumaliza machafuko katika mji mkuu Sanaa. Kulingana na makubaliano hayo itaundwa serikali mpya huku Waziri Mkuu mpya akitarajiwa kuteuliwa katika siku chache zijazo. Waziri Mkuu Mohammed Basindwa alijiuzulu siku ya Jumapili wakati waasi walipoyatwaa majengo ya serikali mjini Sanaa. Watu takriban 140 wameuwawa katika machafuko ya hivi karibuni kati ya vikosi vya serikali na makundi ya waasi.