MBEYA KUGAWANYA: HALMASHAURI YA MBEYA YAPENDEKEZA MKOA MPYA UITWE MBOZIE












BARAZA la madiwani halmashauri ya Mbeya katika mchakato wa kuugawa mkoa wa Mbeya kuwa mikoa miwili imependekeza mkoa mpya uitwe Mbozi ukiwa na wilaya nne.

Map of MbeyaWakizungumza kwa kuchangia kwa zamu wajumbe wa mkitano wa baraza hilo la madiwani wa halmashauri ya Mbeya wamependekeza kuwa mkoa Mpya utakaotokana na kugawanywa kwa mkoa wa Mbeya uite mkoa wa Mbozi.

Mmoja wa wajumbe hao ambaye pia ni diwani wa kata ya Nsalaga Mh. Mashauri Mbembela alipendekeza kwa mkoa wa Mbeya unatakiwa utolewe wilaya za Ileje, Mbozi, Momba na Chunga Maghalibi na uipewe jina la Mbozi.

Alisema kama pendekezo hilo litapita makao makuu ya mkoa huo mpya iwe Vwawa amayo ni makao makuu kwa sasa ya wilaya ya Mbozi, huku mkoa wa Mbeya ukiwa na wilaya za Mbeya, 

Wazo hilo lilipitishwa na baraza hilo la madiwani likiwa chini ya mwekiti wa baraza hilo la madiwani la halmashauri ya Mbeya, Mh. Mwalingo Kisemba amabye pia ni diwani wa kata ya Inyala, Mbeya.

Mh. Mwalingo alisibitisha wazo hilo kwa kupigia kula za kunyosha mkono kwa wajumbe balaza hilo ambapo madiwani wote waliafiki pendekezo hilo.

Mbali na pendekezo hilo la baraza la madiwani wataalam wa ardhi wa halimashauri hiyo walipendekeza mkoa mpya uitwe Rungwe ukibeba wilaya za Rungwe, Mbarali, Kyela na Ileje, 

Ambapo mkoa wa Mbeya ukuwa na wilaya za Chunya, Mbomba Mbozi, na Mbeya huku wakipendekeza wilaya ya Mbeya kugawanyika katika wilaya tatu za ambazo ni Mbeya, Mbalizi na Tembela kitu ambacho  baraza hilo halikuafiki.

Wilaya ya Mbeya baraza limependekeza igawanye katika wilaya mbili na kuwa na halmashauri tatu tofauti na ilivyo kuwa zamani na halmasauri mbili.

Wamependekeza kuwapo na wilaya mpya ya Mbalizi na Mbeya huku halmashauri kuwa ya Mbalizi katika wilaya ya Mbalizi na Mbeya na Jiji katika wilaya ya Mbeya.

Kikao hicho ambacho kilikuwa cha zalula cha kupendekeza mkoa kimekuja baada ya kutolewa tangazo la kupendekeza mkoa mpya uweje na ofisi ya Mkoa wa Mbeya.

  1. Mbeya