WAANDISHI WAJIKITE KUIBUA UKANDAMIZAJI

BI: Kenny Ngomuo akitoa somo kwa waandishi wa habari jijini Mbeya.



WAANDISHI wa habari mkoani Mbeya wametakiwa kujikita katika uandishi wa habari za kiuchunguzi na kuibua ukandamizi unao tokea katika jamii.
 
Rai hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa mtandao wa wanawake na jinsia (TGNP), Kenny Ngomuo wakati akizungunza na baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mbeya katika semina shirikishi juu ya uandishi wa habari za vijijini na kuondoa ukandamizi dhidi ya wanawake.

Ngomuo amesema kuwa wanawake na wanaume  waishio pembezini wamekuwa wakikandamizwa na mfumo dume ulio jengeka katika jamii.

Amesema waandishi wanatakiwa kulivalia njuga swala hilo ili kuikwamua jamii yetu na ukandamizaji wa kijinsia na mfumo dume ambao ukekuwa ukitumikisha upande mmoja na kuacha upande mwingine.

Akitoa mfano wa ukandamizaji kwa jinsia moja unao fanywa na jamii kulingana na utafiti uliofanya na mtandao huo ya TGNP katika kata ya Msewe iliyopo katika halmashauri ya Mbeya alisema kuwa wanawake wamekuwa wakitumikishwa na waume zao.

Alisema wanaume wamekuwa wakiwaachia wanawake kufanya kazi kwa sailimia kubwa hasa utafutaji wa maji ukizingatia upatikanaji wake katika kata hiyo ni mgumu.

Alisema kuwa bali na huduna ya maji pia wanawake wamekuwa wakipata shida katika huduma zingine za kijamii na afya kwa ujumla kitu kinacho ifanya jamii hiyo kuwa tofauti na jamii zingine.

Hivyo aliwataka waandishi kujikita katika uandishi wa kuibua matitizo kama hayo yanayo tokea katika jamii yetu inayo tuzunguka.

Ngomuo alisema kuwa mwandishi wa habari nae ni mwanahalakati wa kupigania haki za wanajanii waishio pembezoni na kuhakikisha wanaibua mambo yaliyo jificha katika jamii za vijijini.