MKOPO UNAPO TOLEWA NA ELIMU YA UJASILIMALI ITOLEWE





MIKOPO ya pembejeo za kilimo inapotolewa wanufaika wanatakiwa kupewa elimu ya ujasiliamali ili waweze kulipa mkopo bila matatizo na kuendeleza kaya zao kulingana na mkopo huo.


Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa wilaya ya Mbarali Adam Mgoyi wakizungumza na wanachama wa Sacoss ya Kapunga Small Holders Sacoss wakati wa kukabidhiwa mkopo wa matrekta 20 yenye thamani ya shilingi 202,112,000 maarufu Powerteller aina ya Kobita kwa ajili ya kuwa na kilimo cha kisasa.

Alisema kuwa wakulima hao wanatakiwa wapatiwe elimu ya ujasilia mali ili kunufaika na mkopo huo kwa kukodisha matrekta hayo kwa wakulima wengine na kijipatia kipato mbadara.

“Wanufaika wa mkopa huu ni lazima wapatiwe elimu ya ujasiliamali ili waweze kujipatia pesa mbadala mbali na kutegemea kilimo katika kulipa mkpo wao” alisema Mgoyi.

Mgoyi alisema wakulima hao wanatakiwa kuyatumia matrekta hayo kama kitegauchumi ambacho watatumia kwa kukodisha na kujipatia pesa mapema na kulipa mkopo huo bila matatizo.

Aidha alitoa wito kwa wanufaiko wa mkopo huo kilipa kwa wakati ili kuijengea uaminifu sakosi yao na kuweza kukopeshwa tena bila kuwa na wasiwasi.

Hivyo amesema kuwa ni vema wakayatunza matrekta hayo ili yawaletee mafanikio hata watakapo kuwa wamelipa mikopo yao na  iwe ni faida baada ya kulipa mikopo hiyo.

Awali mwenyekiti wa Sacoss ya Kapunga small Holder Sacoss  ya Chimala alisema kuwa mkopo huo walioupata unaliba ya asilimia 7 na amewaonya wakulima hao kutunza mkopo huo na kwa sasa hawata ruhusiwa safari kwa umbali mkubwa na matrekta mpaka watakapo maliza kulipa mkoppo wao.

Alisema kuwa  wanufaika hao walisema kuwa watatakiwa kulipa mkopo huo wenye thamani ya zaidi ya Milioni 200 mwaka huu mwezi Juni mwaka huu.

Nae katibu wa sacoss hiyo alisema kuwa serikali inatakiwa kupunguza msongamano katika badari kwani kumekuwa na usumbufu katika uingizaji wa vipuli kwani vifuli hivyo vinatoka katika nchi ziliko nunuliwa powerteller hizo.