TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA



KILA mtanzania anawajibu wa kuitekeleza kauli mbiu ya siku ya Ukimwi yeye binafsi ikifuatiwa na familia yake na kifa kuwa kitaifa ili kufikia malengo ya kauli hiyo.

Akizungumza na Elimtaa Daktari anaye shugurikia masuala ya Ukimwi Mkoani Mbeya Dkt. Sewangi Julius alisema kuwa kauli mbiu ya siku ya
Ukimwi duniani itafukia malengo endapo kila mtanzania ataaza yeye binafsi kutekeleza kauli hiyo ikifuatia katika ngazi ya familia na hatimaye kitaifa.

Alisema kuwa kama mtu mmoja mmoja atasema mimi bila maambukizi ya Ukimwi inawezekana na akahakikisha katika familia yake hauna maambukizi basi taifa bila ukimwi inawekekana.

“Wewe mtanzania kama utajitoa mweneye kupambana na maambukizi ya Ukimwi inawezekana na ukahakikisha na katika familia yako bila ya Ukimwi inawezekana kakika ugonjwa huu hautakuwa tatizo tena la taifa”
alisema Dkt. Julius

Aidha katika suala la kuepuka unyanyapaa na kuutokomeza kabisa alisema kuwa kila mtu akiukataa unyanyapaa yeye kama yeye iwe kwa mwenye maambukizi na asiye na maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi unyanyapaa uta
kuwa hakuna na kutimiza kikamilifu kauli mbiu.

Alisema kuwa mtu mwenye virusi vya Ukimwi kama ata jiamini yeye na kuto jinyanyapaa na asiye na ugonjwa huo itakuwa ngumu kumnyanyapaa
mgonjwa.

Aliongeza kuwa Tanzania bila kuwapo vifo vya watu vitokanavyo na magonjwa nyemelezi inawezekana kama itaanzia kwa mtu mmoja mmoja na
kisha kifamilia na hadi ngazi ya juu.

Hii itawezekana kama kila mtanzania atakuwa na huruma kwa watu wanao ugua na kuwapatia msaada wa karibu na kuhakikisha magonjwa nyemelezi hata wakumbi watu walioona virusi vya Ukimwi.

Alitaja baadi ya magonjwa nyemelezi kuwa ni pamoja na TB ambayo ikitibiwa kwa haraka mtu mwenye maambuukizi ya virusi vya Ukimwi
ataenelea kuishi na kuondoa vifo vinavyo tokana na magonjwa nyemelezi.

“Wito kwa watanzania kuwa makini na magonjwa nyemelezi na kuhakikisha wanawasaidia wagojwa wa Ukimwi kwa kuwapatia vyakila vya lishe ili
kuondoa vifo vinavyo sababishwa na magonjwa nyemelezi” alitoa wito Dkt. Julius.

Alisema siku hii ya Ukimwi inayo fanyika kila Mwaka disemba mosi kwa mkoa wa Mbeya maadhimisho hayo yana fanyika leo katika wilaya ya Mbozi
Mkoani Mbeya.

Katika kuasimisha siku hiyo ya Ukimwi ikiwa imebebwa na ujumbe mzito ‘Sifu tatu, hakuna maambukizi, hakuna unynypaa na hakuna vifo vya
mangonjwa nyemelezi’ na kupitia maadhimisho haya kutatolewa huduma ya upimaji bure na elimu mbali mbali kuhusiana na maambukizi ya ugonjwa
huo.

Hiyo amewandishi kutumia vyombo vya habari kufikisha elimu kuhusiana na magonjwa ya ukimwi na jinsi ya kujikinga na ugojwahuo na njia za
kuepuka magonjwa yanayo ambatana.

Mwisho