KEMEKUWA na serikali nyingi za vijiji ambazo hazisomi mapato
na matumizi ya fedha na kutokuwa na miradi ya ambayo itaingiza mapato katika
vijiji vyao.
Serikali nyingi za vijiji hapa nchini zinashidwa kufanya
mambo ya kimaendeleo kutokana na kutokuwa na mradi inayo igiza pesa katika
mfuko wa kijiji hatimaye kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake menyekiti
wa kijiji cha Ruanyo kata ya Igurusi wilayani Mbarali mkoani Mbeya, Righton
Mwakitwange, alisema kuwa katika kijiji kukiwa na mradi unao kisaidia kupata
pesa kinaweza kuendelea kirahisi hivyo kuwapo ulazima wa kusoma mapato na
matumizi.
Alisema kuwa Jumatano ya wiki hii katika kijiji chake
anatarajia kusoma mapato na matumizi katika mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Mwakitwange alisema katika mkutano hua anatarajia
kujadiliana na wananchi kuunda miradi mbalimbali ya kuipatia halmashauri ya
kijiji hicho ambapo mpaka sasa uongozi wa kijiji una mpango wa kujenga eneo la
kuegesha magari makubwa.
Hivyo katika mkutano huo watalileta suala hilo kwa wananchi
ili wajue kuwa kutakuwa na ujezi wa kitegauchumi hicho ambacho kitaingiza fedha
katika kijiji na halmashauri ya wilaya ya Mbarali.
Alisema ujezi wa eneo hilo la kuegesha magali lita saidia
watu wengine kuwekeza katika huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo nyumba za
kulala wageni na maduka mbalimbali na vijana kupata ajira.
Katika kijiji hicho ambacho hakina vitegauchuni vya kutosha
amesema kutokana na upungufu huo wamekuwa wakikwama katika ujenzi wa shule ya
kijiji ambayo mpaka sasa wamejenga madarasa ambayo kwa sasa inahitajika
kuezekwa nipo walipo kwamia.
Alisema kama kijiji kingekuwa na miradi ya kutosha wangeweza
kukamilisha ujenzi wa shule hiyo mapema na amewataka wananchi ambao ni wakazi wa kijiji hicho walioko nje ya
Mbeya wajitokeze katika uchangiaji wa kijiji chao na kufanya maendeleo kusonga
mbele.
mwisho