Kuhusu kifo cha
msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga
akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza
mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea
akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es
salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na
kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
Kamanda amesema hakuna kona
kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo
Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali
salama kwa sababu haitembei.
SIKILIZA KAMANDA WA POLISI ALIVYOSIBITISHA KIFO CHA SHARO MILIONEA
SIKILIZA KAMANDA WA POLISI ALIVYOSIBITISHA KIFO CHA SHARO MILIONEA