Libya leo inafanya uchaguzi kwa mara ya kwanza
ambao ni huru na wa haki katika kipindi cha miaka
60.
Uchaguzi huo ni wa bunge ambalo litaunda serikali mpya baada ya miongo minne ya utawala wa kidikteta wa kanali Muammar Gaddafi.
Wapiga kura watachagua wabunge 200 ambao nao watamchagua Waziri Mkuu na Baraza la mawaziri kabla ya kufanyika kwa uchaguzi kamili mwakani chini ya katiba mpya.
Uchaguzi huo unaambatana na visa ambapo watu wenye silaha wamefunga vituo vya mafuta kwenye eneo la mashariki wakidai Libya yenye mfumo wa shirikisho.
Waandamanaji na waasi wa zamani wametishia kuususia uchaguzi huo.
Wanadai kuwa mgawanyo wa viti vya ubunge umewekwa kwa ajili ya kuupa upande wa magharibi kiti cha mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli, na hivyo kuwa na nguvu kuliko mashariki.