JAMII mkoani Mbeya imetakiwa kuzingatia usafi wa mazigira
kwa ajili ya afya na kizazi kijacho kikute mazingira mazuri.
Hayo yamebainishwa mwishoni mwa wiki hii katika maadhimisho
ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa klabu ya wanamazingira wa shule ya sekondali
Mbeya day, na Gerald Mwenyekiti wa mazingira mkoa wa Mbeya.
Amesema jamii iyalinde mazingira kwa kupanda miti na usafi
mwingine wa kimazingira na mazingira kututunza sisi.
Pia amewataka wanafunzi kujituma katika kuhamasisha utunzaji
wa mazingira, katika klabu ya Mbeya sekondari katika kuazimissha siku hiyo ya
mazingira wamepanda maua katika shule yao na kwenda kuwatembelea wagonjwa
katika hospitali ya mkoa na kuwapelekea matunda.
