WAKAZI WALALAMIKIA MABWAWA YA MAJI TAKA


WAKAZI  wa eneo la Rumbila kata ya Iwambi  wameuomba uongozi wa kata na halmashauri ya jiji kuweza kulitafutia ufumbuzi suala mabwawa ya maji kwa kupiga dawa ya kuuwa mbu ili kuweza kunusuru afya zao .

Akizungumza na wandishi wa Elimtaa mmoja wa wakazi katika eneo hilo Bw. Rashid Mwakipete amesema kuwa wanapata madhara makubwa kwani mbu wengi wamezaliana katika mabwawa hayo na hivyo kupelekea tatizo la ugonjwa wa maralia .


Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Gabriel Mwamwasi  amesema kuwa tatizo hili ameweza kulifikisha katika ngazi husika  pamoja na uongozi wa idara ya maji safi na maji taka mkoani hapa  na uongozi umefika mara chache na nyunyizia dawa kwa ajili ya kuuwa vimelea vya mbu.


Hata hivyo ameongeza kuwa uongozi umewataka wananchi wawe wavumilivu kwani muda si mrefu mabwawa hayo yatakaushwa naytanza kutumiwa mabwawa yaliyoko katika eneo la Kalobe jijini hapa.

Aidha Mwamwasi amesema kuwa suala la kutupa taka katika korongo lililopo jirani na eneo la mabwawa analipiga marufuku na kuwaasa wananchi waache mara moja ,na pia ameahidi kujitahidi  kumwaga kifusi cha udongo katika eneo hilo ili liweze kufukiwa . 
Joice Milambo