MBEYA: MLIMA MBEYA SASA NI MLIMA TAI


MLIMA Mbeya umepewa jina lingine baada ya kupandwa na wanafunzi wa chuo cha Talent Informative TAI mpaka kileleni na kukutana na wakazi wa maeneo hayo na kuuita Mlima TAI.

Akizungumza na Rock Fm mkurugenzi wa wa chuo hicho, Erick Komba amesema kuwa wameubatiza jina hilo ili ikiw ni moja katika mradi wao wa kutambulisha vivutio vya utalii vya Mbeya katika uso wa dunia.

Amesema katika mradi wao unaoitwa Mbeya online watazunguka katika vivutio vyote vya Mbeya na kuanzisha bonanza litakalo fanyika katika mlima Mbeya ambao kwa sasa wanauita mlima TAI.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa wameamua kufanya hivyo katika harakati za kuutangaza mkoa wa Mbeya na vivutio vyake vya utalii.

Mbali na kupanda mlima Mbeya katika program yao ya Mbeya Online wa tahakikisha wanatembelea vivutio vyiote kama vile Dalaja la Mungu la Rungwe na Lile la Mbozi ili kuuonyesha ulimwengu kwamba kuma vivutio vingi katika mkoa wa Mbeya ambavyo havipo popote duniani.

 

Amesema watatembelea pia katika ziwa Ngosi ambalo linadaiwa kutokea kimaajabu kabisa na hakuna mnyama anayeishi huko zaidi ya Bata.

 

Akitoa historia fupi ya ziwa Ngosi amesema ziwa hilo lilitoka Rungwe na kuhamia maeneo ya Igawilo Mbeya Vijijini.

Komba amesema kuwa hivi karibuni kutakuwa na bonanza la kuhamasisha utalii katika mkoa wa Mbeya na kuutambulisha ulimwengu uzuri wa Mkoa wa Mbeya na vivutio Vyake.

 

Amesema Jina hili la mlima Tai ambao zamani ulikuwa Mlima Mbeya si la ajabu ila ni kawaida kwani Mwanjelwa Inaitwa Dox, Mbeya inaitwa Green City kwahiyo kubadilika kwa mlima huo si kitu cha ajabu masikioni mwa watu.

 

Komba amesema wameamua kufanya hivyo kama uzalendo na kuwavuta watalii wengi kutokana na kufunguliwa kwa kiwanja cha Ndege cha kimataifa hivi karibuni na kuufanya uwanja huo kuwa bize wakati wote.