KAMPUNI ya
Access computer ya jijini Mbeya imepania kujikita zaidi katika kudhamini
michezo na burudani, ili kuboresha na kuinua kiwango cha fani hizo mkoani Mbeya
na nchi nzima kwa ujumla.
Akizungumza
na super Star jana mfanya biashara mashuhuri anayemiliki kampuni ya Access
Computer Limited, Samweli Mtela, alisema kuwa kampuni yake imedhamilia
kudhamini michezo mbalimbali ili kuibua vipaji vipya kwa maendeleo ya mkoa wa
Mbeya.
Samwel enock
mtela alizaliwa tarehe 2-8mwaka 1974 katika sehemu ya ilembo mkoani mbeya ,na
anatoka katika familia ya kikristo ya Baba Enock Mtela,na mama Neema Mtela.
Alianza
shule mwaka 1984 katika shule ya msingi Shilanga iliyopo Mbeya Vijijini na
mwaka 1985 alihamia shule ya msingi Mwenge ya Mbeya mjini na kumaliza darasa la
saba shuleni hapo mwaka 1990.
Alisema kuwa
mnamo mwaka 1991-1994 alisoma katika shule ya sekondari ya Meta na kuhitimu
kidato cha nne .
Baada ya
kuhitimu kidato cha nne alianza masomo ya kompyuta kwenye chuo kilichopo eneo
la Block Q mjini Mbeya mwaka 1995 ambapo alisoma kipindi cha mwaka mmoja.
Mfanya
biashara huyo ambaye pia ni mwanamichezo mashuhuri aliongeza kuwa ,katika mwaka
wote wa 1996 alikuwa akifanya shughuli zake za kibiashara hapo mjini Mbeya.
Mwaka
uliofuata aliajiriwa na chuo cha mafunzo ya kompyuta kilicho kuwa chini ya
taasisi ya Elimu ya watu wazima hadi mwaka 2002 alipo hitimu masomo yake.
Akiwa bado
mwajiriwa wa taasisi ya Elimu ya watu wazima alikuwa pia akichukua mafunzo ya
kompyuta katika chuo cha sayansi na teknolojia cha MIST ambacho zamani
kilijulikana kama Mbeya Technical College (MTC).
Kuanzia mwaka
2003 alifungua ofisi ya ufundi wa Kompyuta na vifaa vingine vya ofisini,na
kudumu katika kazi hiyo hadi ilipofika
mwaka 2006.
Mwaka mmoja
baadae alianza rasmi kujishughulisha na mambo ya Kompyuta ,mashine
za kudurufu pamoja na utengenezaji vifaa
vingine vya ofisini .
Alisema
kuanzia hapo hadi sasa ameendelea na kazi hiyo ambayo imemuwezesha kusonga
mbele kimaisha,na kupata changamoto nyingi zinazo msukuma kuboresha huduma kwa
jamii.
Mwaka jana
kampuni hiyo ilijiingiza katika udhamini wa mambo ya budani na michezo kama
vile mpira wa miguu,ili kuibua vipaji vipya kwa wanamichezo chipukizi kwa
maendeleo ya mkoa wa Mbeya.
Aliitaja
michezo mingine anayoidhamini kuwa ni pamoja na mpira wa Pete,waigizaji wa
Filamu pamoja na mashindano ya ulimbwende.
Kampuni hiyo
mwaka jana ilidhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana walio chini ya
umri wa miaka 17,na kushikisha timu 12 za jijini Mbeya.
Mashindano
mengine aliyodhamini yalijulikana kama Mastara Cup yaliyofanyika katika viwanja
vya shule ya msingi ya mwenge,yakiwepo mashindano ya Ligi Ya Taifa ngazi ya Wilaya
kwa timu zote za daraja la tatu mjini Mbeya.
Mshindi wa
kwanza wa mashindani hayo alijipatia fedha taslimu shilingi laki tatu,seti ya
jezi na mpira mmoja,wa pili alipata shilingi laki mbili,seti ya jezi na mpira
mmoja wakati mshindi wa tatu alijipatia shilingi laki moja na nusu,seti ya jezi
na mpira mmoja.
Alizitaja
gharama nyingine za kuendeshea mashindano hayo kuwa ni gharama za waamuzi na za
uwanja,ambazo jumla yake ilikuwa sh.Mil.5.
Kampuni hiyo
mbali ya kudhamini michezo hiyo pia inajihusisha na kutoa huduma kwa watoto
yatima ,misaada mingine Makanisani
,shuleni na vyuoni.
Mtela ametoa
wito kwa wadau wa michezo nchini kujitokeza kudhamini michezo hiyo ili kukuza
na kuibua vipaji vipya kwa vijana ambao wanaweza kumudu maisha yao kupitia
michezo kama ajira.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
