BROWN ATOA USHAHIDI DHIDI YA DREKE

Mwanamuziki wa R&B Chris Brown amezungumza na polisi wa jijini New York, NYPD, kuhusiana na ugomvi uliotokea kwenye bar na uliomsababishia jereha kwenye kidevu.

Mtandao wa TMZ umeambiwa kuwa mwanasheria wake ameipa NYPD “ushahidi wa macho” unaodai kuwa rapper Drake alihusika kwenye varangati hilo.

Mtandao huo umesema umeambiwa kuwa mwanasheria wa Chris, Mark Geragos,ameenda jana NYPD kukabidhi ushahidi unaoonesha kuwwa Drake na Meek Mill walimshambulia.

Pia umedai kuwa Drake amekuwa akishirikiana na polisi japo haujui kama ni yeye ndiye aliyeongea nao japo inaonesha kuwa wawakilishi wake ndio waliozungumza na polisi.