BAJETI MWAKA HUU NI TRILIONI 15

 Waziri wa fedha na uchumi Dk William Mgimwa jana amewasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ambayo ni sh Trilioni 15 tofauti na ile ya mwaka unaomalizika ya Sh Trilioni 13.5

Bajeti hiyo ina vipaumbele 7 ambavyo ni Miundombinu, kilimo, viwanda, rasilimali watu, huduma za jamii, utalii, pamoja na biashara ya ndani na nje na huduma za fedha.

Moja kati ya mapendekezo ya udiferenti yasema kuwa :- Ukitaka kuweka jina kwenye gari badala ya Plate number itakugharimu shilingi milioni 5 nayo itadumu kwa muda wa miaka mitatu.


Bajeti imelenga kuviwezesha viwanda vya ndani kuhimili soko la ushindani kwa bidhaa zake dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.


Bajeti imetoa pendekezo la kulinda kazi za wasanii kwa kusajili kazi hizo ili kuwaingizia faida ya kipato kitakacho wawezesha kunufaika na kazi zao.
Hayo ndiyo ya udiferenti lakini pia ukweli ni kuwa inaonekana kama bajeti haina vitu vipya sanaaa, na imekaa kimjini mjini (isiyona manufaa kwa walio vijijini ) na baadhi ya vipengele vyake ni kama kuna marudio ya vile ambavyo vimewahi semwa huko nyuma kama ya kutuchapa bakora kwenye vinywaji na vileo .