Mkataba huo utaruhusu wanajeshi 10,000 kusalia Afghanistan
Siku moja baada ya kuapishwa kwa rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani, serikali yake imetia saini mkataba mpya wa usalama na shirika la kujihami la NATO.
Mkataba
huo utaidhinisha zaidi ya wanajeshi elfu kumi na mbili, wengi wakiwa
wamarekani, kusalia nchini Afghanistan hata baada ya kumalizika kwa
kandarasi yao mwaka huu.
Mkataba huo ulitiwa sahihi katika hafula
iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni na mshauri wa maswala ya
usalama wa kitaifa wa Afghanistan Hanif Atmar na balozi wa Marekani
nchini humo Jim Cunningham, huku Rais mpya wa Afghanistan Ashraf Ghani akishuhudia.
Rais Ghani ametia sahihi mktaba huo na Marekani
Uhusiano kati ya Marekani na Afghanistan ulizorota kutokana na Rais aliyeondoka, Hamid Karzai, kukataa kutia sahihi mkataba huo. China
ya masharti ya mkataba huo, ni chini ya wanajeshi 10,000 wa Marekani
wanaotarajiwa kubaki nchini Afghanistan ili kutoa mafunzo na msaada kwa
wanajeshi wa taifa hilo.
Rais aliyeondoka Hamid Karzai alikataa
kwa muda mrefu kusaini mkataba wa kuwaongezea wanajeshi wa Marekani muda
wa kukaa huko, na hivyo kusababisha mvutano kati yake na Marekani.
Aliyekuwa rais wa Hamid Karzai alikataa kata kata kutia sahihi mkataba huo
Bwana Karzai alikuwa
anasisitiza kuwa la muhimu zaidi ni kuanzisha mpango wa amani na
kusitisha mapigano na wanamgambo wa Taleban.
Vikosi vya NATO vimekuwa vikipunguzwa nchini Afghanistan na taratibu kurudisha udhibiti wa usalama wa nchi hiyo kwa vikosi vya Afghanistan.
Marekani imeukaribisha mpango wa kugawana madaraka uliomtangaza waziri wa fedha wa zamani Ashraf Ghani kuwa rais mpya wa Afghanistan, na kutumai kwamba mkataba na Marekani kuhusu ulinzi, uliokumbwa na utata utatiwa saini wiki ijayo. Ghani na mpinzani wake Abdulla Abdulla walitia saini makubaliano hayo siku ya jumapili na kumaliza miezi mitatu ya uchaguzi ulio na utata ulioikwamisha nchi hiyo wakati ambapo wanajeshi wa kigeni wanaoongozwa na Marekani wakimaliza muda wao wa takriban miaka 13, wa mapambano dhidi ya wanamgambo wa Taliban. Serikali ya muungano nchini Afghanistan inatoa nafasi ya makubaliano ya pamoja ya usalama yatakayotoa nafasi ya kuwepo kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan baada ya kumaliza muda wao mwishoni mwa mwaka huu, jambo ambalo rais anayeondoka Hamid Karzai alikataa kulitia saini. Kulingana na makubaliano hayo Abdulla Abdulla atachukua nafasi mpya ilioundwa ya mtendaji Mkuu ambayo ni sawa na ile ya Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amesema leo kuwa anaunga mkono
juhudi za Afghanistan za kutafuta amani na Taliban na kwamba atawasaidia
wajumbe kukutana na kamanda mmoja wa zamani wa kundi hilo. Akizungumza akiwa mjini Kabul baada ya kukutana na Rais wa Afghanistan
Hamid Karzai, Sharif amerudia usemi wake kuwa serikali yake ilimwachia
kamanda wa zamani Mullah Baradar, ambaye anazingatiwa na Afghanistan
kama ni mtu muhimu katika kulileta kundi la Taliban kwenye meza ya
mazungumzo. Ziara hiyo ya siku moja ni ya kwanza kwa Sharif tangu
alipochukua uongozi mwezi Mei na inajiri wakati Karzai akiwa katika mzozo wa
hadharani na Marekani kuhusiana na mpango muhimu wa usalama unaohusu
jukumu la majeshi ya Marekani yatakayosalia Afghanistan baada ya NATO
kuondoka mwaka ujao. Sharif pia amekutana na Baraza Kuu la Amani nchini
Afghanistan, ambalo linataka kuanzisha mazungumzo na wanamgambo wa
Taliban ambao wamekuwa wakipambana na jeshi la NATO linaloongozwa na
Marekani tangu mwaka wa 2001.