Njombe kuanza kuchakata vizazi mviringo

WAJASILIAMA mkoani Njombe wameanza kujiongeza kwa kuanza na kuondokana na kuuza viazi ambavyo vinamagana sasa wameaza kuuza viazi vilivyo menywa na kuvicharanga katika vipande vidogo vidogo tayari kwa kupika Chips kwa kutumia mashine na kuwauzia waandaaji vya vyakula kwa wingo kama Sherehe, Migahara na hoteri mkoani humo.
Wajasiliamali hao wanasema kuwa wamegunua kuwa awali wateja wao walio kuwa wakiwauzia viazi vilivyo menywa lakini vilikuwa havija katwa na kuuza vingine vikiw ana Magana wamegundua kuwa wanaweza kuongeza thamani ya viazi kwa kuvimevya na kuvicharanga.
Kabla ya kuanza kutumia mashine ya kucharanga viazi katika umo moja walikuwa wakitumia visu na kutumia muda mwingi kuandaa viazi kidogo lakini sasa wanaweza kuanda viazi vingi na kutumia muda kidogo.
Licha ya kutumia muda mwingi katika uandaaji wa viazi majeraha katika vidore vyao ilikuwa ni sehemu ya maisha yao kutoka na na visu walivyo kuwa wakivitumia kucharanga viazi baada ya kuviondoa madanga.
“Sasa tumepata mashine ya kucharanga viazi katika saizi moja inatupunguzia muda sisi kama wajasilimali wadogo na tunatumia nusu saa kwa debe moja la viazi (kuilo 20) wakati zamani tulikuwa tukitumia saa moja na nusu kwa ujazo huo huo,” Alisema Mjasiliamali Evelina Evaranstino
Evaranstino Aliongeza kuwa kama kuna mtu anaweza kuwasaida kupata Jokofu kwaajili ya kutunia viazi vilivyo menjwa wanaseza kuwa wanasafirisha viazi vilivyo menjwa na kuuza nje ya mkoa wa Njombe badala ya kusafirisha vile vilivyo na maganda na maranyingine kuharibikia njiani.
Pamoja na kuwa vimemenywa Sala Chaula mkazi wa Idundilanga Njombe alisema kuwa bado wanauza bei sawa na ile ya vile vya maganda kwa kuwa bado ndio wanaingia katika soko hivyo hawajaanza kuuza bei kubwa.
Alisema kuwa sasa watu wanao uza chips mitaani na wale wenye hoteli wanaenda kununua kwao na kuwa wamekuwa wakiwarahisishia umenyaji na kuomba kujitokea kuwasaidia kutoa mawazo ya mbinu za uhifadhi zaidi wa viazi.
Mashine hiyo ya kucharanga viazi katika umbo moja kwaajili ya chipsi imetolewa ka kikundi hicho cha wanawake wajasiliamiali na Mbunge wa Njombe Mjini Edward Mwalongo ikiwa ni kuunga mkono vikundi vinavyo ongeza thamani ya mazao.
Akizungumza baada ya kukabidhi mashine hiyo Mwalongo alisema kuwa viwanda sio mpaka kuanza na mitambo mikubwa lakini wanaanza kwa kuwa na mitambo nidogo na wakisa ona faida ya kutumia mitambo midogo watajiongeza na kuanza kununua mashine kubwa na kupanua masoko.
“Dar es Salaam hawachukui viazi kwaajili ya mbegu kwa kuwa wanachukua kwaajili ya kula mnaweza kuondoa maganda na kuuza viazi vilivyo menywa na mkaondokana na masuala ya Lumesa” Alisema Mwalongo.