BOMOA BOMOA NJOMBE, MABANDA YAVUNJWA

WAKAZI wa mtaa wa Idundundilanga maeneo ya Chaugingi halmashauri ya Mji na Mkoa wa Njombe Nyanda za juu kusini mwa Tanzania wameishutumu serikali kupitia darali ambaye anaondoa vibanda vya wafanyabiashara wadogo pembezoni mwa barabara za mji huo kwa kuto toa elimu kwa wafanyabiashara juu ya zoezi hilo la uvunjaji wa vibanda na meza za biashara.

Wakizingunza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa zoezi hilo limekuwa ghafla kwa kuwa awali wakipatiwa taarifa za uondoa vibanda vyao hawakuambiawa waondoe meza pekee na wengine wakisema hawakuambiwa muda wa kuondoa vibanda vyao.

Aidha baadhi ya wakazi wa mtaa huo ndio walikuwa wanategemea kununua mboga mboga katika mitaa hiyo wanasema kuwa soko linakotakiwa kuwepo ni mbali sana na makazi yao bora kama kila mta ungekuwa na soko ili huduma za mahitaji wazipate hapo.

Kiongozi wa zoezi hilo ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya udalali ya Igagara Kawe Msango anasema kuwa Mji utakuwa safi kwa kufanywa na wakazi wenyewe na haiwezekani mji ukasafishwa na wageni ndio maana wapo kazini kufanya kazi hiyo ili kuweka mji safi kwa niaba ya mkurugenzi.


Katika zoezi hilo Mgamo walio chini ya kampuni hiyo wamefanya shuguri zao wakiwa na mashoka kwaajili ya kuangusha mabanda yoto na kuvunja meza zilizo sehemu isiyo rasimi.

READ MORE.........Bonyeza hapa kwa Video zaidi ==> VIDEOZ