Hekta 9400 zateketea Njombe Wilaya ya Njombe, Mwaka jana mwaka huu matukio 9

WAKULIMA miti ya mbao mkoani Njombe hatarini kuacha kupanda miti kutokana na miti hiyo wanayo panda kila mwaka kukumbwa na moto kichaa ambao huiterketeza ikiwana umri tofauti na kuanza upya ama kufa kabisa.
Mwaka jana na mwaka huu moto umetokea katika maeneo mbalimbali Mkoani Njombe, kwa mujibu wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mwaka jana zaidi ya Hekta 9400 katika katukio tofauti 19 wakati mwaka huu mpaka sasa kuna matukio 9 ambapo ukubwa tathimini inaendelea kufanyika.
Mwenye mamlaka na misitu halmashauri ya wilaya ya Njombe anasema kuwa matukio ya moto yamekuwa yakitokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kuandaa mashamba ugomvi lakini ili kudhibiti matukio ya aina hiyo tayari kunahatua ambazo zimeanza kuchukuliwa.

Wataalamu wa misitu na mazingira wanasema kuwa pamoja na kuteketea kwa misitu na kusababisha hasara za kiuchumi kwa wakulima wa misitu kuna madhara kwa wanama na wadudu wa porini na kusababisha pia mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkoa wa Njombe ni baarufu kwa ukulima wa miti ya mbao ambayo huingiza mapato jamii na serikali za halmashauri kwa mkoa huu lakini kwa sasa sokoni mbao ni nyingi  wasiwasi ni ubora wa mbao hizo kwa kuwa miti inayo vunwa ni kwasababu imeungua na sio kwakuwa imekomaa.