VYAMA VYA UPINZANI WAANZA KUMDAI MRITHI WA PROF. MUHONGO

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, ambae ni Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, akiongea katika mkutano wa hadhara Jumatano 2/8/2017 eneo la Goba mwisho katika Jimbo la Kibamba, amemtaka Rais Magufuli ateue Waziri wa Nishati na Madini ili aongoze majadiliano kuhusu madini.
“Ni muda mrefu umepita Rais hajateua Waziri wa Nishati na Madini, ambaye ndiye anayestahili kuongoza majadiliano kuhusu madini, badala yake anamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kuongoza majadiliano kuhusu masuala ya madini, Ameamuachia Waziri wa Katiba na Sheria kwa sababu alikuwa kwenye tume ya mabadiliko ya Katiba, nae amekataa kuendeleza mabadiliko ya katiba mpya” amesema Mnyika.
Amesema Serikali makini isingeanza na makinikia huku madini yanaendelea kuchimbwa na kutoka, wakati kuna makampuni mengine yanaendelea na uchimbaji, na kampuni inayoingoza kwa uzalishaji ni kampuni ya Geita Gold mine (GGM) na inaendelea na uchimbaji hakuna ufuatiliaji wala majadiliano yeyote yanayoendelea, huku Taifa likielekezwa kwenye majadiliano kuhusu makinikia badala yafanyike majadiliano kuhusu madini kwa upana wake.

from Blogger http://ift.tt/2vwccA7
via IFTTT