UKITAKA KUSTAAFU MAPEMA ZINGATIA MAMBO HAYA.

  • Watu wengi sana wanatamani kuwa na uwezo na uhakika wa kustaafu mapema, lakini ni wachache sana wanachukua hatua mahususi kuhakikisha wanalitimiza jambo hilo.
  • Ili uweze kustaafu mapema, mambo matatu yanahitajika: kipato cha uhakika, kuweka akiba na kuwekeza akiba yako.
  • Jambo la kuzingatia ili utimize lengo hili ni kufanya mambo hayo matatu yawe ndio kipaumbele chako maishani.
  • Vijana wanajulikana kwa kuwa na tabia ya kutopenda kufata sheria, na linapokuja swala la matumizi ya pesa zao wanazozipata kwa jasho lao – wengi zaidi huwa hawataki hata ushauri kabisa.

    Lakini uwezekano wa kustaafu mapema unaweza kuwafanya wengi washawishike kuachana na ubishi wao na kufikiria uhakika wa maisha yao ya uzeeni na kuanza kuchukua hatua za uhakika kuyanyoosha wangali bado vijana na wenye nguvu za kufanya kazi.

    Image result for GRAND PARENTS

    Zifuatazo ni njia hizo na jinsi ya kufanya:

    1. Tengeneza chanzo imara cha mapato
    Kama huna chanzo cha mapato, hutakuwa na nafasi hata ya kuanza kujenga utajiri. Hatua ya kwanza kabisa ya kuhakikisha unapata uhuru wa kipato ni kuwa na chanzo cha uhakika cha kipato ili uwe na uhakika kwamba kutokana na kipato hicho, unaweza kuweka akiba pamoja na kuwekeza kwa ajili ya maisha ya baadaye.

    Kwa baadhi ya watu, hii yaweza kumaanisha ufanye kazi kwa ufanisi kwenye ajira yako ya sasa ili uweze kutimiza lengo hili. Ukiwa na chanzo cha uhakika cha mapato, hata ikiwa ni kutokana na kazi za mkataba au tenda za kulipwa kwa siku, bado unaweza kuweka mipango ya baadaye na kuanza kuitekeleza, japo kidogo kidogo.

    2. Weka akiba sehemu kubwa ya kipato hicho
    Ukishakuwa na kipato cha uhakika, jambo muhimu ni kuhakikisha kuwa hutumii pesa yote unayopata. Kujifunza jinsi ya kuishi maisha ya gharama nafuu chini ya kipato chako ni muhimu ili uweze kubaki na pesa (hasa ukianzia ujanani mwako) na uweze kujiwekea akiba itakayokusaidia kwa maisha yako yote yaliyobaki.

    kwanza, miongoni mwa njia rahisi zaidi za kuhakikisha utakuwa na fedha uzeeni mwako ni kujiunga na mfuko wa hifadhi za kijamii. Mifuko hii itakusaidia kutoa michango yako kila mwisho wa mwezi au kwa muda maalum na kuja kuipata utakapotimiza umri wako wa kustaafu. Kwa waajiriwa, michango hii huwa inakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mshahara wako – kwahiyo huna haja ya kuwa na wasiwasi kuhusu hilo – lakini kwa ambao hawajaajiriwa, unaweza kujiunga kwenye mifuko hii kama mtu binafsi, kwakuwa inaruhusiwa kufanya hivyo pia. Michango unayoiweka ni kiasi kidogo sana cha pesa kwa mwezi, lakini faida yake uzeeni ni kubwa.

    Pia, unaweza kupunguza matumizi yako ya pesa kwa kupunguza gharama za nyumba (kama umepanga) ili kodi yako kwa mwezi isizidi asilimia 30 ya kipato chako.

    3. Wekeza akiba yako kwenye vitega uchumi vitakavyoongezeka au kutopungua thamani
    Kuwa na pesa nyingi kwenye akiba yako ni jambo zuri, lakini unapoiwekeza pesa hiyo yaweza kusababisha tofauti kubwa sana kwenye safari yako ya kustaafu mapema.

    Kuna wanaoamua kuwekeza kwenye sekta ya majumba, na inaweza ukunufaisha kwakuwa una uwezekano wa kuingiza kipato cha kila mwezi kutokana na kodi za pango.

    Kwa wale wasiovutiwa na biashara ya majumba, unaweza kujifunza na kuwekeza kwa kununua hisa za makampuni mbalimbali ambayo yana rekodi nzuri ya ukuaji.

    Mwanzo wa safari ya mafanikio ya kuwa na uhuru wa kipato unaanza kwa uamuzi wako kwamba kufanya hivyo ni muhimu sana kwako. Kisha ukiwa unazingatia malengo yako, basi unaweza kutimiza kila unachokitaka bila wasiwasi.

from Blogger http://ift.tt/2vYuBW9
via IFTTT