Watu 4 Wanashikiliwa Na Polisi Mkoani Morogoro Kwa Tuhuma Za Kukutwa Na Dola Bandia Na Gongo Lita 268

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watu nane kwa tuhuma za kupatikana na dola bandia za kimarekani 66 ambazo kama zingekuwa halali kila moja
ingekuwa na thamani ya dola mia moja, pombe haramu ya gongo lita 268, simu za magendo, chaja pamoja na betri zake. 
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Urlich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti akiwemo mfanyabiashara Haji Athumani
aliyekuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea Makambako akiwa na simu 748 za aina mbalimbali, betri 650 za simu na chaja 830 akiwa kazihifadhi kwenye mfuko wa
sandarusi bila kuwa na stakabadhi kuonesha uhalali wa bidhaa hizo. 
Katika tukio jingine jeshi hilo la polisi linamshikilia Mwajuma Said mkazi wa Tungi akiwa na dola bandia 66 za kimarekani ambapo kama zingekuwa halali kila moja
ingekuwa na thamani ya dola 100, mabunda tisa ya makaratasi yaliyotengenezwa mfano wa fedha sambamba na watuhumiwa wengine sita zaidi kwa kutengeneza na
kuuza pombe haramu ya Gongo ambapo lita 268 za pombe hiyo na pikipiki iliyokuwa ikisafirisha vimekamatwa.

from Blogger http://ift.tt/2veUnCW
via IFTTT