VITU VIWILI AMBAVYO BILIONEA WARREN BUFFETT HUVIWEKA KWENYE POCHI YAKE MUDA WOTE

Bilionea katika sekta ya uwekezaji, Warren Buffett yupo katika nafasi ya nne ya watu matajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa zaidi ya dola za Marekani bilioni 73 kwa mujibu wa jarida la Bloomberg. Lakini pamoja na kiwango hiki kikubwa cha utajiri alichokuwa nacho, bado huwa anasifika kwa kupenda vitu ambavyo watu wengine wanaviona vidogo sana, au havina thamani.
Jarida la habari za kibenki la GOBankingRates lilimhoji bilionea huyo na kusema kuwa kwenye pochi yake kuna vitu huwa anaviweka muda wote, na akavitaja vitu viwili ambavyo huwa havitoi kabisa. Cha kwanza ni picha za kumbukumbu, picha za watoto wake na wajukuu zake walizopiga wakiwa utotoni. Cha pili ni noti ya dola 50 aliyopewa na mmiliki wa benki ya ‘Berkshire Hathaway’ iliyopo Rockford katika jimbo la Illinois ambayo ina sahihi ya mmiliki wa benki hiyo kama ambavyo noti huwa na sahihi za Rais wa nchi.
“Walitengeneza noti yao wenyewe, kwahiyo huwa natembea nikiwa nayo kama ishara ya kujiombea niwe na bahati,” Buffett aliliambia jarida la habari za kibenki la GOBankingRates.
Katika kipindi cha nyuma, Buffett alikuwa akijaza noti za dola 100 kwenye pochi yake, kadi maalumu inayomruhusu kula bure kwenye mgahawa wowote wa McDonald mjini Omaha, Nebraska na kadi ya American Express ambayo ilitengenezwa mwaka 1964.
Buffett haweki vitu anavyovithamini kwenye pochi yake tu. Ofisini kwake, sio tu kwamba anatumia meza ile ile iliyokuwa inatumiwa na baba yake, lakini ameweka treni ya plastiki iliyopo juu ya reli aina ile ile ambayo baba yake alikuwa anaiweka kwenye meza hiyo.
Hii ni kumbukumbu kwake kwamba Buffett tunayemuona sasa anamkumbuka na kumjali shujaa wake, ambaye ni baba yake mzazi.
“Sijawahi kumuona baba akifanya lolote — katika maisha yake yote ambalo — lisingekufanya ujisikie vizuri utapoliona kwenye kurasa ya mbele ya magazeti,” alimwambia mwandishi wa kituo cha CBS, Charlie Rose alipotembelea ofisi za bilionea huyo mwaka 2012. “Alikuwa mtu mzuri sana.”
Kwenye kuta za ofisi yake kuna vipande vya makala za zamani zilizochapishwa kwenye gazeti la New York Times na cheti alichopata kwa kuhudhuria kozi ya mkufunzi maarufu, Dale Carnegie.
Makala hizo, ambazo zinaelezea kwa kina mshtuko uliotokea nchini Marekani mwaka 1907 na anguko kuu la uchumi, zinafanya kazi ya kuwa hadithi za kumpa tahadhari bilionea Buffett. “Niliona niweke ukutani siku za mshtuko mkubwa uliotokea kwenye soko la hisa la Wall Street kama kumbukumbu kwamba chochote kinaweza kutokea duniani,” alisema kwenye makala ya kipindi cha televisheni cha HBO kilichoitwa “Becoming Warren Buffett (Kuinuka kwa Warren Buffet).”
Cheni alichoweka kina maana kubwa sana kwake binafsi: Kinamkumbusha kozi aliyohitajika kujifunza na kumuwezesha kushinda woga mkubwa aliokuwa nao wa kuongea mbele ya kadamnasi, ambayo Buffett anasema kuwa ilibadilisha kabisa uelekeo wa maisha yake moja kwa moja.

from Blogger http://ift.tt/2eQcXNZ
via IFTTT