VIPODOZI VYENYE SUMU VILIVYOZUIRIWA VYAKAMATWA

Idara ya Afya katika Manispaa ya Songea imekamata vipodozi na vyakula vyenye sumu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili. Akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea, Afisa Habari wa Manispaa hiyo, Albano Midelo amesema kuwa vipodozi hivyo vimekamatwa katika kipindi cha kuanzia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu katika ukaguzi endelevu unaofanywa na idara hiyo.
Alitaja vipodozi vyenye sumu ambavyo vimekamatwa kuwa ni Actif Plus, Betasol, Broze, Cocoderm, Carolight, Carotene, Citrolight, Clairmen, Cocopulp, Corton, Diproson na Epiderm.
Vingine ni Extralair, Jaribu, Lemonvate, Mekako, Miki, Montclair, Movate, Naomi, Oranvategel, Perfect, Princess, Rapid, Sabuni Protex, Seven Miracles, Toplemon, Whiteplus, Dodo, Teint, Super Clair, Greeting, 14 days, Dermotyl, Natural, Gold Touch, Coco Dermbetacort, Extral White, Formula Avas, Lemon Cream na Diva Maximum.
Midelo amesema kuwa katika ukaguzi huo, pia vimenaswa vipodozi halali ambavyo vimemalizika muda wake vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano.
Vipodozi halali vilivyokamatwa ambavyo muda wake kimatumizi umeisha ni Skin Soft, Puer Glycerine, Royal Touch, U & Me na Mambo Fresh.
Idara hiyo pia imekamata vyakula vilivyokuwa vinauzwa na wakati muda wake umekwisha vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu.

from Blogger http://ift.tt/2uFPvta
via IFTTT