Sahau kuhusu Lukaku, hawa nao waling’ara walipovua jezi ya Chelsea

Romelu Lukaku ni mchezaji ambaye hakuwa na thamani kubwa sana kama alivyopaswa kuwa nayo wakati akiwa Chelsea, kocha wa sasa wa United na jopo la ufundi la Chelsea lilisema Lukaku hakuwa bora sana na ndio maana wakamuondoa katika kikosi chao.
Maisha yanakwenda kasi sana baada ya Lukaku kujiunga tu na West Bromich moto ukawaka na kiwango kikakua sana, alipoenda Everton ndio kabisa kila klabu ikatamani kuwa naye, sasa kama ulizani ni Lukaku tu ambaye aaling’ara baada ya kuondoka Chelsea utakuwa umekosea.
Daniel Struridge.Alionekana sio lolote akiwa Chelsea na mwaka 2013 akaona sio kesi ni bora aende zake Liverpool, amekuwa na kiwango kizuri sana akiwa na klabu ya Liverpool japokuwa majeraha ya mara kwa mara yamekuwa yakimuweka nje ya uwanja,lakini pamoja na majeruhi yote hayo ila katika mechi 119 Sturidge ameshapasia kamba mara 60.
Ryan Bertand.Tetesi zinasema klabu ya Chelsea iko katika mpango wa kumrudisha mlinzi huyu wa kushoto lakini bado kuna vilabu kama Sevilla na Napoli nao wanataka saini ya Bertand, wakati alipokuwa Chelsea naye alionekana wa kawaida sana na hakuwa na thamani lakini akiwa na Southampton amekuwa kati ya walinzi wanaozungumziwa sana katika ligi kuu Uingereza.
Nemanja Matic,Mwaka 2009 alijiunga na klabu ya Chelsea lakini hakupewa nafasi sana aliishia kucheza michezo mitatu, baadae Chelsea wakaona sio mtu sahihi kwao wakaamua kumpeleka Benfica akitumika kama chambo ya kumpata David Luiz hiyo ilikuwa mwaka 2012 lakini kufikia mwaka 2015 Chelsea hao hao wakauona uwezo mkubwa kwenye miguu ya Matic na wakaamua kumrudisha kwa £21m.
David Luiz.Kama unakumbuka Luiz aliletwa Chelsea baada ya Matic kupelekwa Benfica,lakini Chelsea nao wakaona wamuuze kwenda PSG na baadae wakamfuata tena kumnunua, tangu arudi Chelsea ni ukweli usiopingika kwamba Luiz amekuwa mhimili mkubwa sana wa ngome ya ulinzi ya Chelsea na kufanikiwa kubeba kombe msimu uliopita.
Juan Cuadrado.Baada ya mashindano ya kombe la dunia la mwaka 2014 watu wengi waliuona uwezo wa Mcolombia huyu na akafanikiwa kutua Chelsea,kilichotokea huko ni kati ya hadithi chungu kwake kwani aliishia kusota benchi na baadae Chelsea hao hao wakaamua kumtoa kwa mkopo kwenda Juventus na baadae kumuiza kabisa lakini maisha ya Cuadrado akiwa Juventus yamekuwa matamu kwake kama mchezaji akiisaidia Juventus kubeba makombe Italia na kucheza fainali ya Champions League.
Mohamed Salah.Walipomnunua toka Basel hata mashabiki wa Chelsea walitamani kuona ubora wake lakini ghafla akaoneshwa mlango wa kutokea Darajani, umri wa Salah bado ulikuwa mdogo wakati akiwa Chelsea lakini hawakutaka kumpa muda, msimu uliopita alikuwa bora sana na As Roma akifunga mabao 15 na kuassist 11 jambo lililowavuta Liverpool kumrudisha Epl.

from Blogger http://ift.tt/2ul71Tj
via IFTTT