RONALDO ATHIBITISHA JUU YA TETESI ZA MPENZI WAKE KUWA NA UJAUZITO WA MTOTO WA NNE

Mshambuliaji wa Real Madrid na nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana alithibitisha tetesi zilizoenea kwamba mpenzi wake ana ujauzito ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu kuzaliwa kwa mapacha. Huyu atakuwa ni mtoto wa nne kwa staa huyo wa soka.
Ronaldo aliliambia gazeti la El Mundo la nchini Hispania kwamba “nina furaha sana” kwakuwa anatarajia kupata mtoto mwingine, na sasa hivi mtoto huyo atakuwa na mpenzi wake wa sasa Georgina Rodriguez. Habari hizi amezitoa ikiwa ni mwezi mmoja tangu kuzaliwa kwa mapacha Mateo na Eva, ambao pia kama kwa kaka yao Cristiano Jr. ambaye kwa sasa ana miaka 7, mama yao hajawekwa wazi.
Katika mahojiano hayo, mwandishi alimuuliza swali: “Wanao wanaendeleaje?”
“Ni wazuri, nafurahia sana,” alijibu Ronaldo.
“Je, una furaha pia kwakuwa wengine yupo njiani?” aliuliza mwandishi ambapo Ronaldo alijibu: “Ndio, tena sana.”
Tetesi za mrembo huyo kuwa na mimba zilipingwa vikali na mama yake baada ya kuripotiwa na picha iliyopigwa na mapaparazi waliokuwa wakiwafatilia wakiwa mapumzikoni.
Katika akaunti yake ya mtandao wa Facebook, Jumatatu iliyopita Ronaldo aliweka picha wakiwa kwenye mgahawa kwenye visiwa vya Ibiza na kuandika kuwa: “Nitawapa habari kubwa hivi karibuni!!”. Kwenye picha hiyo ya familia, Ronaldo ameonekana pamoja na Cristiano Jr., dada zake Elma na Katia Aveiro, kaka yake Hugo, mama yake Maria Dolores na mpwa wake Rodrigo. Georgina pia alikuwepo kwenye picha hiyo hivyo kufanya habari hizi za uthibitisho kuwa tamu zaidi.

from Blogger http://ift.tt/2uc9JIj
via IFTTT