Picha: Watu watatu wauawa kwa kuchomwa moto kwa tuhuma za wizi wa pikipiki wilayani Kahama

Wananchi waliojichukulia sheria mkononi jana wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama, mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku kuamkia jana baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa jana majira ya saa nne asubuhi.
Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa jana baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.
Afisa Mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.
Miili ya marehemu hao imechukuliwa na jeshi la polisi wilaya ya Kahama na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya wilaya ya Kahama.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tpeJZO
via IFTTT