METHOD MWANJALE ACHAGULIWA KUWA NAHODHA WA KLABU YA SIMBA

Benchi la ufundi la klabu ya Simba chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu, beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwenye mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu, Mohammed Hussein (Tshabalala) na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.
Klabu inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi, Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa Timu.
Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden
Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
IMETOLEWA NA..
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA

from Blogger http://ift.tt/2vbwyhQ
via IFTTT