MANJI AONDOLEWA MUHIMBILI USIKU CHINI YA ULINZI MKALI

Mfanyabishara maarufu nchini Tanzania Yusuf Manji ameondolewa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akitibiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi na kupelekwa Gereza la Keko lililopo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la MTANZANIA zilizothibitishwa na wakili wake, Manji anayetuhumiwa kwa mashtaka 7 ya uhujumu uchumi na usalama wa taifa ambayo hayana dhamana aliondolewa hospitali hapo juzi usiku.
Taarifa kutoka Gereza la Keko na ndani ya JKCI alikokuwa akitibiwa zimethibitisha kuwa Manji ambaye pia ni Diwani wa Mbagala kwa tiketi ya CCM, amepelekwa Keko.
Gazeti hilo limeeleza zaidi kuwa, jana viunga vya taasisi hiyo ya matibabu havikuwa vimezungukwa na Askari kama ilivokuwa siku za nyuma Manji alipokuwa ndani.
Alipotafutwa Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Prof. Janab alikataa kuzungumzia suala hilo akisema kuwa ni kinyume na maadili ya kazi kutoa taarifa za mgonjwa.
Alipoulizwa wakili anayemtetea Manji, Hudson Ndusyepo alisema ni kweli ameruhusiwa (Manji) kutoka hospitali na kuthibitisha kuwa ni kweli yupo Gereza la Keko lakini yeye hajui ni muda gani aliporuhusiwa kutoka.
Manji pamoja na wenzake watatu mapema wiki huu (Julai 5) walisomewa mashtaka 7 chini ya sheria ya uhujumu uchumi na usalama wa taifa baada ya kukutwa na vitambaa vya sare za jeshi pamoja na mihuri mali zinazodaiwa kupatikana kinyume na sheria lakini pia kutishia usalama wa taifa.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Quality Group, Deogratius Kishinda (28), Mtunza Stoo, Abdallah Sangey (46) na Thomas Fwere (43).
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sXN14n
via IFTTT