KOREA KUSINI YATOA VIDEO INAYOONESHA WANAWAKE WA NCHI HIYO WALIOFANYWA WATUMWA WA NGONO

Korea Kusini imetoa kile inachokitaja kuwa kanda yake ya kwanza ya video iliyorekodiwa mwaka 1944 ikionesha wanawake wa nchi hiyo waliolazimishwa kuwa watumwa wa ngono na wanajeshi wa Japan wakati wa vita vya pili vya dunia.
Kanda hiyo iliyorekodiwa na wanajeshi wa Marekani nchini China, ilipatwa na wachunguzi waliofadhiliwa na serikali ya Korea Kusini katika chuo cha Seoul kwenye kumbukumbu za Marekani (US National Archives).
Askari wa Japan akikagua wanawake hao kwenye danguro
Kanda hiyo ya sekunde 18 inaonesha wanawake kadha wa Korea Kusini wakiwa wamejipanga wakizungumza na mwanajeshi wa China.
Wanaharakati nchini Korea Kusini wanakadiria kuwa wanawake 200,000 walilazimishwa kufanya kazi katika madanguro ya wanajeshi wa Japan wakati wa vita kuu ya pili ya dunia.
Askari wa Japan wanatuhumiwa kuwafanya watumwa wa ngono wanawake wa Korea Kusini
Wanaaminika kutokea nchini Korea, lakini pia kutoka nchini China, Indonesia , Ufilipino na Taiwan.
Hadi sasa kumbukumbu za wanawake waliolazimishwa kuwa watumwa wa ngono na wanajeshi wa Japan wakati wa vita vya pili vya dunia imekuwa ni picha na ushuhuda.
Tazama video hiyo:
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t5mTop
via IFTTT