TETESI: MTAA WA “VICTOR WANYAMA” DAR WAFUTWA

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, imeufuta mtaa uliopewa jina la mchezaji wa Kimataifa wa Kenya katika Kata ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kamati ya Kata ya Ubungo jana ilimpa mtaa Victor Wanyama ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Kenya na kiungo wa Tottenham Hostpurs ya nchini Uingereza ambaye yupo nchini kwa mapumziko.
Taarifa za kufutwa kwa mtaa huo zimeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku ikiwa imenukuu Kitengo Cha Habari na Uhusiano cha Manispaa ya Ubungo.
Taarifa hiyo inasomeka, “Majina ya mitaa hupendekezwa na kamati za mitaa husika kisha hupelekwa kwenye vikao vya WDC vya Kata halafu maamuzi ya WDC hupelekwa kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kuingizwa kwenye kikao Cha kamati ya Fedha na uongozi, Baraza la Madiwani, halafu DCC, RCC na Kisha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na baadaye kwa Mchapaji mkuu wa serikali na mwisho hutokea kwenye Tangazo la serikali GN.”
Aidha taarifa hiyo ilieleza zaidi kuwa, taratibu za kubadilisha jina la mtaa ndizo hizo hizo.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuthibitisha au kukanusha madai hayo ambayo yamewasikitisha wengi hasa mashabiki wa mpira.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2u39Ww5
via IFTTT