Steve Nyerere: Mimi Sijaigiza Sauti za Mbowe na Wema, Sio Kwa Kiingereza Kile..

Steve kakanusha kuhusika na uigizaji wa sauti za mtongozo zilizovuma baina ya watu wanaodaiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mrembo Wema Sepetu wa Bongo Movie..
Steve Nyerere
“Kwanza mimi toka nimeanza kuigiza sauti sijawahi kuigiza sauti za viongozi wa chama fulani, Pili, kutongoza napo sio dhambi, ni sunna (akimaanisha ni jambo jema tu kwa mwanaume yoyote kulifanya). 
Tatu, sio kila kitu ambacho kimefanywa na familia fulani basi Steve anahusika. 
Limenikera na kuniumiza sana. Pia sio kwa Kingereza kile cha kubembeleza vile, nina uwezo huo? Na pia sio mimi peke yangu ninayeweza kuigiza sauti za watu, waigizaji wapo wengi.” alinukuliwa akisema Steve Nyerere.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sX7LtB
via IFTTT