Rais Magufuli Awafunda Wakuu wa Mikoa..Awataka Kuwanyang’anya Hati za Umiliki Watu Wenye Mashamba Makumbwa..!!

Rais wa Tanzania John Magufuli amewaagiza wakuu wote wa mikoa Tanzania Bara kuongeza juhudi za utatuzi wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa kuwanyang’anya hati za umiliki watu wenye mashamba makubwa ambayo hawayaendelezi.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo, Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Wakuu hao wa mikoa, Tanzania ambacho kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi na baadhi ya Mawaziri.
“Mashamba yote yaliyotelekezwa, fuateni taratibu za sheria, yanyang’anyeni wapewe Watanzania ambao wapo tayari kuyaendeleza, lakini fanyeni jambo hili kwa kufuata utaratibu,” Rais Magufuli.
Aidha Rais amewaagiza Wakuu wa Mikoa wote kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa viwanda katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi kuongeza thamani ya mazao yao na kuzalisha ajira.
Rais Magufuli amesema kila Mkuu wa Mkoa anapaswa kufanyia kazi fursa za uanzishaji wa viwanda katika eneo lake na kuhakikisha anashawishi wawekezaji kuzitumia fursa hizo kama inavyofanyika katika Mkoa wa Pwani ambako tangu Awamu ya Tano iingie madarakani viwanda vikubwa 83 vimejengwa na vingine kukamilika huku viwanda vidogo zaidi ya 120 pia vikiwa vimejengwa.

ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s9fGEZ
via IFTTT