RAIS MAGUFULI ATOA ZAWADI ZA SIKUKUU YA EID EL-FITR

Rais John Magufuli ametoa zawadi za Eidd El Fitri zenye thamani ya Sh10.9 milioni kwa vituo tisa vya wenye mahitaji maalumu vya Mkoa wa Dar es Salaam.
Pia, ametoa zawadi hizo katika vituo viwili vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.
Zawadi hizo zimekabidhiwa leo (Jumamosi) katika mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon Panga kwa niaba ya Rais.
Panga amezitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengi.
“Mheshimwia Rais kwa upendo wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwamo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa katika makazi, ili washerehekee sikukuu hii vizuri ,” amesema Panga.
Pia, amevitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Rais kuwa ni kwa upande wa Jiji la Dar es Salaam kuwa ni Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry­ Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke na Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization).
Vingine ni Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.
Vile vile, amevitaja vituo vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Makao ya Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home, Mkuranga – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Karibu Nyumbani, Kibaha – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma na Shule ya Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.
Vituo vingine ni Mahabusu ya Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto – Sinyanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Magugu – Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.
Kwa upande wa Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake – Pemba na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.
Utoaji wa zawadi hizo ni utaratibu unaofanywa na marasi wa awamu zote zilizopita zilizopita
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s51yQ0
via IFTTT