RAIS KIKWETE AELEZA CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO KWENYE KULIMA MANANASI

Pwani. Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.
Akizungumza leo Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.
“Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu,” amesema.
Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.
“Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,”amesema.
Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.
Mwananchi
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2stqErg
via IFTTT