Nawashangaa Mnaonifananisha na Used, Mimi Niko Bikira– Ebitoke

Mchekeshaji kutoka Timamu African Media, Ebitoke baada ya kutangaza anamuhitaji msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol katika mahusiano ya kimapenzi, leo ameibuka na kioja kingine.
Ebitoke ambaye amekuwa akitoa vichekesho mbali mbali kupitia mitandao ya kijamii, ametoa kauli ambayo imetafsiriwa kuwa hajawahi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote.
“Nawashangaa mnaonifananisha na USED, mimi niko SEALED jamani,
#Hatufanani thamani yangu ni kubwa kuliko make up za kichina,” aliandika Ebitoke Instagram.
Baadhi ya mashabiki wake wamechukulia jambo hilo kama utani, wengine wakimpongeza, huku wengine wakibeza kwa kudai amejishusha kusema hivyo.

from Blogger http://ift.tt/2rPymJL
via IFTTT