Matokeo ya michezo mikubwa ya kirafiki hii leo.

Timu ya taifa ya Brazil ikiwa ugenini dhidi ya Australia ilitoa kipigo kikubwa cha mabao 4 kwa 0 dhidi ya Australia huku mabao ya Brazil yakiwekwa kambani na Diego Souza, Thiago Silva, Taison na Diego Souza.
Argentina nao walikuwa ugenini dhidi ya Singapore walishinda mabao 6 kwa 0 huku mabao ya Argentina yakifungwa na Fredrico Fazio na Joaquin Correa waliofunga kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili yaliongezwa mengine manne Gomez,Daniel Parades,Lucas Alario na Di Maria.
Waafrika wenzetu Bafanabafana walikuwa nyumbani kuikaribisha Zambia na Zambia waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja huku mabao ya Zambia yakiwekwa kimiani na Brian Mwila na Lubinda Munia huku la kufutia machozi la Bafanabafana likifungwa na Lebongang Manyama.
Mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya Cameroon walifungwa mabao 4 kwa 0 na Colombia huku mabao ya Colombia yakifungwa na Rodriguez,Yery Moina akifunga mawili na Jose Izquirero huku Cameroon wakimaliza pungufu baada ya Ndip Tambe kupewa kadi nyekundu.
Mabao mawili ya Harry Kane hayakutosha kuizuia England isifungwe mabao 3 kwa 2 na Ufaransa ambao mabao yao yalifungwa na Samuel Umtiti,Djibrii Sidibe na Osmane Dembele katika mchezo ambao Ufaransa walimaliza pungufu baada ya Raphael Varane kuoneshwa kadi nyekundu,
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rq7D9t
via IFTTT