JE ni Kweli Pesa za Kale Zina Nguvu za Kichawi?

Moja kwa moja utawaza kuhusu rupia(rupee ya mjerumani) na pesa nyingine za kale na yale yanayosemwa kuzihusu hasa kwenye habari nzima za kichawi
Watu wamezinguka na kuzinguliwa hasa watu wametapeliwa na wengine kufa wakitafuta hivi vitu vinavyotajwa kuwa na thamani kubwa
Ukweli huu hapa na si pesa tu bali na vitu vingine vya kale
1. Aina ya malighafi iliyotumika
Wakati huo vilitengenezwa vitu imara sana kutokana na upatikanaji wa malighafi ya kutosha …vitu kama vyombo vya bati na chuma urembo kama bangili mikufu pete nk leo hii ukivipata na kuviyeyusha kila kimoja unaweza kutengeneza kumi kupitia hicho kimoja
2. Uhifadhi
Wajerumani kwa hapa kwetu walikuta malighafi vito na madini ya kutosha sana! Kutokana na uhifadhi hafifu wakati huo vingi ya hivi vitu viliwekwa tu majumbani mwao wakiviandaa kuvidafirisha kwao
Vita ya pili ya 1939-45 iliwachanganya mno na walipoelekea kushindwa waliamua kuficha mali yote kwenye mashimo makubwa mashambani misituni kwenye mahandaki na milimani kusikofikika kwa urahisi kisha wakawaua watu karibia wote walioshiriki na wanaojua yale maficho wakasepa
Huku kote mali hizo zilihifadhiwa kwenye vyumba imara vilivyojengwa kwa zege gumu hasa ili iwe ngumu kuchimbua ama kuvunja na kama ni mapangoni yalikuwa mapango ya mbali hasa milimani na misituni
3. Dhana ya majoka na viumbe wa ajabu
Huko kwenye hayo maficho kuna baadhi ya watu walisalimika hivyo wakasimulia vizazi vilivyofuata
Kizazi cha kusaka utajiri wa haraka kikaona fursa na kuamua kuchangamkia dili. ..Wajerumani hawakuweka ulinzi wowote wa majoka! Hao ni viumbe tu walijitwalia makazi huko ambako ndio maisha yao yaliko
Watu walioenda bila tahadhari waliumwa na hayo madubwana na kupoteza maisha! Waliosalimika walitimua mbio na kuunda stories za kufikirika
4. Dhana ya uchawi na majini
Kwa wale waliosaka kwenye mahandaki na mashimo marefu yenye vyumba vilivyojengwa kwa zege , baada ya kufanikiwa kuvunja hayo mazege na kutaka kuingia ndani nao walikutana na mauzauza ya kila aina
Unajua ni kwa nini? Sehemu yoyote yenye mfumo wa nyumba ama chumba isiyokaliwa na binadamu roho zinazotangatanga na mapepo hufanya makazi yao kumbuka ile mada ya kutakasa makazi! Hivyo ukiingia huko lazima ukutane na vitu vya ajabu…Mjerumani hahusiki kabisa!
5. Uamuzi wa kufanya kafara ama tambiko kabla ya kuchimba ama kuingia pangoni
Wengi walitafuta waganga wa kienyeji kwenye hili na hawakufanikiwa. ..waliofanikiwa walifanikiwa kwa ujanja tuu….ukienda kwenye pango misituni ukachinja mnyama ukapiga manyanga automatically mkiondoka ile nyama italiwa na kuna wakati manyanga huleta kelele na kufukuza mnyama yoyote aliyeko pangoni…ndio maana baada ya kafara hamuingii siku hiyo hiyo bali kesho yake nk
Wale wa kwenye mashimo NA mahandaki ni ibada tu ya kuziomba roho ziondoke ama kuzifukuza kwa kutumia mitishamba na harufu wasizozipenda….mkikutana na roho korofi mtachezea kichapo mpaka muache kila kitu na kutimua mbio kali sana
6. Ukweli hasa ni UPI?
Baada ya vita ya pili kukoma na baadae Uhuru wajerumani walishindwa kurudi kwa ubabe hivyo wakatumia njia za kijanja kurudi
Unajua waliondoka na ramani zote kule mali zilikofichwa hivyo walirudi kuzichukua kwa njia ya kununua yale maeneo na kuyaendeleza kwa kujenga shule vyuo hospital nk ama miradi ya barabara ufugaji na kilimo
Kwa njia hii walichukua vyao kiulaini mno
7. Thamani na umaarufu wake ni UPI?
Vitu vya kale kwa wenzetu vina thamani kubwa sana….wenzetu wana utaratibu wa kuweka vituo vya antiques na kuchaji watalii pesa ndefu kuviangalia . kila kimoja kinakuwa kimeandikiwa historia yake. Kwa hiyo wakija huku kuvitafuta wengi huenda kuviuza kwenye hayo maduka kwa bei kali mno
8. Nguvu ya utajiri
Biashara imevamiwa , vitu vya kale haviwezi kukupa utajiri wa miujiza ..havina huo uwezo bali kuna baadhi kutokana na malighafi iliyotumika kuvitengeneza vina mvuto kwenye ulimwengu wa giza kama mabangili ya shaba
9. Usumbufu
Kuna watu wanawachezea wenzao shere na kuwasumbua bila sababu.. Miaka hiyo pesa ilitengenezwa kwa mpango maalum(nadhani hata sasa) na zilitengenezwa kwa miaka… Kuna miaka pesa hazikutengenezwa. Sasa mtu anakupa dili na kukuahidi kukupa pesa ndefu ukimletea rupee ya mwaka fulani Rupie_robo_DOA_1913.JPG
10. Hitimisho
Kuna baadhi ya sehemu kulikofichwa hizo mali wafichaji walinuizia ama kufanya mambo ya giza ili atakayejaribu kuchukua ama apate madhara au asizione kabisa…lakini kwa sehemu kubwa ni habari zilizotiwa chumvi nyingi

from Blogger http://ift.tt/2sEsFk3
via IFTTT