Hongera Viongozi wa CHADEMA, CCM Walitaka Kupoka Hoja Yenu ya Mikataba

Kumekuwa na juhudi za makusudi kutaka kuwaaminisha Watanzania kuwa wapinzani wanatetea wezi wa Madini wakati walioshirikiana na wezi wanajulikana wakiwemo Wabunge wa CCM waliopitisha sheria mbovu kwa kura za NDIYO. Tume ya rais imewaumbua.
Jana MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari amempongeza rais JPM na kumfananisha na Rais wa Kwanza wa Ghana, Kwame Nkrumah na Waziri Mkuu wa Kwanza wa Congo (DRC), Patrice Lumumba kutokana na juhudi binafsi anazofanya kutetea rasilimali za nchi.
Wakati huohuo Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema ambaye pia alikuwa mgombea urais UKAWA, Mh. Edward Lowassa amesema, juhudi zinazofanywa na rais ni za kuungwa mkono na Watanzania wote, akaongeza kuwa anachofanya rais ndicho alichokuwa anakihubiri kwenye kampeni, ila akamshauri pamoja na mazuri anayofanya kiungwana anatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kwa niaba ya chama chake CCM kwa kusaini mikataba mibovu ya kinyonyaji.
Kila mtu anajua CHADEMA/UKAWA, Lissu, Mnyika, Zitto ndiyo wenye hoja yao tangu mwanzo, CCM na washangiliaji wao Team Makinikia walikuwa wamedandia treni kwa mbele.
Naomba kuwaambia wanaCCM wote sasa tulieni kimya watetezi halisi wa Madini wameamua kujitokeza, mnachotakiwa ni kutubu badala ya kuendelea kujifanya mna uchungu na madini wakati mliyagawa wenyewe.
Hongera viongozi wa CHADEMA, tunaomba viongozi wengine zaidi wajitokeze ili kuwafundisha CCM maana halisi ya uzalendo usioyumba.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2szJmxx
via IFTTT