HII NDIYO SHULE YA MSINGI ANAYOFUNDISHA MSANII ROMA MKATOLIKI

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Ibrahim Mussa (Roma Mkatoliki) amegeukiwa kufundisha ambapo jana aliibukia katika Shule ya Msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam na kufundisha wanafunzi wa darasa la saba somo la hisabati.
Msanii huyo akiongea na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa anafundisha somo hilo kwa wanafunzi wa darasa la saba kwani wengi hufeli kutokana na kuwa na walimu.
  • “Mimi kitaaluma ni mwalimu wa hisabati, kutokana na kufeli mno somo hilo nimeanza kampeni ya kufundisha na kugawa vitabu kwa kuanza na shule hii kwa sababu pia nitakuja kufanya onyesho la muziki kwenye sikukuu ya Eid kwa mara ya kwanza,” alisema Roma.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ramadhan Mashaka alisema kuwa msanii huyo amepata kibali cha kufundisha shuleni hapo.


“Nimekagua na kugundua kuwa Roma ni mwalimu mzuri wa hisabati hivyo tumemkaribisha afundishe wanafunzi bila hofu, tukiwa na imani kubwa kuwa wataelewa kwa sababu wanafundishwa na mtu wanayempenda na hii itaongeza morali ya wanafunzi shuleni hapa,” alisema Mwalimu Juma.

Licha ya kufundisha, atafuturisha watoto yatima wa Kituo cha Nira kilichopo Mbagala Chamazi na atatoa zawadi za sikukuu ya Eid.

from Blogger http://ift.tt/2t62JvI
via IFTTT