Gor Mahia wamejihakikishia kucheza na Everton

Timu ya Gor Mahia imefanikiwa kutwa taji la michunuano ya SportPesa Super Cup 2017 baada ya kuifunga AFC Leopards kwa mabao 3-0 ikiwa ni mchezo wa ‘Mashemeji derby’ uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Ushindi huo umewapa Gor Mahia kombe la SportPesa Super Cup pamoja na fursa ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton ambao watakuja Tanzania mwezi Julai katika ziara yao ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi ya England maarufu kama England Premier League.
Gor Mahia wameondoka na kiasi cha dola za Marekani 30,000 zaidi ya shilingi 58 milioni za Tanzania wakati mshindi wa pili AFC Leopards wao wakiondoka na dola 15,000 zaidi ya nilioni 22 za Tanzania.
Kocha mtanzaniaambaye ni kocha msaidizi wa AFC Leopards amekubali kwamba walizidiwa katika kila idara na kufanikiwa kuuteka mchezo.
“Leo hatukuwa vizuri, ukiangalia dakika 20 za kwanza Gor Mahia walitawala katika kila idara. Kupambana mchezaji mmojammoja tulipoteza na hadi mapumziko tulikuwa 0-0 , kipindi cha pili nacho hatukuanza vizuri na walipopata goli baada ya hapo wakatawala mchezo na kuongeza magoli mengine.”
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2ssZGjI
via IFTTT