DIAMOND ATOBOA SIRI YA MTOTO WAKE ALIYEKO MWANZA

Mkali wa muziki wa Bongo fleva nchini, Diamond Platnumz, hatimaye ametoboa siri ya maisha yake baada ya kueleza kwamba ana mtoto wa miaka saba aliyezaa na mwanamke anayeishi jijini Mwanza ambaye alikuwa naye kwa usiku mmoja tu.
Akizungumza na redio moja, Diamond alisema kuwa mtoto huyo alimpata baada ya kwenda mkoani humo kufanya shoo ya muziki.
Alisema kuwa awali alikuwa akiwasiliana na mwanamke huyo, kabla ya kupoteza mawasiliano baada ya kumpata mpenzi mwingine ambaye alimlewesha kimahaba.
“Nina mtoto jijini Mwanza, sijui kama yupo kwani sijamuona tangu azaliwe kutokana na mama yake kushindwa kunitumia picha. Nakumbuka siku moja nilipokwenda huko nilikutana na mama yake, akaniambia kuwa amezaa mtoto lakini kila ninapomwambia anitumie picha hataki,” alisema Diamond.
“Siku moja nilimuuliza kama kajifungua lakini akakataa, baadae nikaja kuambiwa ana mtoto lakini kila nilipomuomba nimuone alikataa.”Diamond hakuwahi kumtaja mwanadada huyo mwenye mtoto wake.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8LdcX
via IFTTT