Di Maria ahukumiwa kwenda jela mwaka mmoja

Wakati kashfa ya ukwepaji kodi ikiwaandama Wareno wawili maarufu ambao ni Cristiano Ronaldo na Jose Mourinho kumeibuka lingine ambapo Angel Di Maria naye amekumbwa na mkasa kama huo.
Di Maria amekiri kuhusika na ukwepaji kodi ambapo alifanya tukio hilo kati ya mwaka 2010 na 2014 akikwepa kuriba kodi kiasi cha euro 1.14million.
Di Maria inasemekana baada ya kugundua kwamba amefanya kosa hilo aliamua kupanga njama na baadhi ya watu wa mamlaka za kodi ili kosa lake lisijadiliwe.
Baadae polisi waliamua kuingilia kati suala hilo na kuanza kumchunguza upya Di Maria ambaye alipochunguzwa sana alikiri mbele ya sheria kwamba alifanya kosa hilo.
Di Maria alikiri pia kutumia akaunti mbili ambazo ndizo alikuwa akizitumia kukwepea kodi na kila akaunti inamfanya kuhukumiwa miezi 6 jela na hivyo kuhukumiwa miezi 12 jumla na kulipa faini ya 60%.
Lakini Di Maria hatakwenda gerezani kwani sheria za Hispania hazimpeleki gerezani mtu aliyehukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili haswa kama hajawahi kufungwa hapo kabla na Di Maria atatumikia kifungo cha nje.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rU9TpV
via IFTTT