AUDIO: Aibu, Anaswa nyumbani kwa Mtu akiwa Utupu Makete

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani Makete mwishoni mwa wiki walipigwa na butwaa baada ya mwananchi aliyejulikana kwa jina la Waziri Anyingisye (38) kukutwa akiwa utupu nyumbani kwa mtu asubuhi ya Juni 11 mwaka huu
Baadhi ya wananchi wamelihusisha tukio hilo na imani za kishirikina kwa kuwa si la kawaida, ambapo alikutwa nyumbani kwa Christon Mbilinyi (24) ambaye ni katekista majira saa 10 alfajiri mtaa wa Ikiligano kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo Tarafa ya Matamba wilayani Makete
Akizungumza nasi kwa njia ya simu Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Bw. Christopher Fungo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba mabli na yote yaliyotokea walihakikisha mtuhumiwa huyo hakudhuriwa na umati wa watu waliofika eneo la tukio kushuhudia
Naye diwani wa kata ya Kitulo kilipo kijiji hicho Mh. Asifiwe Mahenge amesema baada kutokea kwa tukio hilo alitoa taarifa kwa jeshi la polisi wilaya ya Makete ambao walifika eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi
Kwa upande wa jeshi la polisi ambao walifika eneo la tukio wamesema baada ya mahojiano na mtuhumiwa huyo katika kituo cha polisi hakuna ushahidi wowote ambao mpaka sasa umeonesha mtuhumiwa huyo ni mchawi kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kwa kuwa hakukutwa na shanga au matunguli kama ilivyozoeleka
Aidha jeshi hilo mpaka sasa linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa usalama wake ambapo pia limedai kumkuta mtuhumiwa huyo akiwa amevaa tisheti ya rangi ya bluu na nyeupe huku chini akiwa mtupu
Sikiliza sauti za tukio hilo kwa kubonyeza play hapo chini>>>>>>>
http://ift.tt/2srebVv
http://ift.tt/2t0PT1N ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s05r7q
via IFTTT