Umewahi Kukaa Sehemu Ukawa Unapiga Story na Mungu? Fanya Hivyo kwa Njia Hii…!!!

Je umewah kukaa sehemu ukawa unapiga story na Mungu mnacheka,mnagonga na kushauriana?
wakati mwingine dhambi zetu zinatutenga na Mungu tunaanza kuwa waoga na wenye kujishtukia, wenye chuki kwa Mungu na moja kwa moja tunajitenga naye. lakini kama Tungejua vile ambavyo yeye alipenda tuwe wala tusingekuwa tunamchukulia jinsi tunavyomchukulia. Mungu alipenda sana tuish naye kwa maisha ya amani na upendo. 
sasa chukua muda wako vizuri nenda chumbani kwako katika mazingira mazuri na tulivu. kama utakaa kwenye kochi au kitandani au hata chini yeye Mungu hampi shida ongea naye. anasikiliza. na unaweza ukawa unaongea na Mungu kiasi kwamba sometime unajikuta unacheka au unapata furaha flan ambayo katika mazingira ya kawaida huwez ipata. Unapoongea na Mungu Ukamzoea utajikuta ukiwa unapiga naye story moyoni unajisikia utulivu sana. kichwani kunakuwa hakuna makelele tena hata kama humo ndani kuna makelele. 
unasikia harufu nzuri yenye utulivu na mwili mwako unalegea kwa maana ya kuwa una relax sana. ukimya wake unakuwa kana kwamba hata mapigo ya moyo huyasikii. hapo unaweza jikuta unatulia sana. una furaha sana, una amani sana. utaongea na Mungu. 
give thanks and praise. Acha lawama na majungu unapokuwa unapiga story na Mungu
Usiongee na Mungu kwa Kumlaumu. nani anapenda lawama? hamna. na ni unaweza anzisha naye mazungumzo kwa lawama? nenda kwa boss wako anayekupenda na kukujali. mwambie ” boss unajua wewe unatunyonya sana?hutujali, kazi nyingi mshahara kidogo, tunateseka na kazi zako wewe tu ndo unafaidika” halafu angalia uhusino wenu utakuaje.
Mpe sifa Mungu. maana Mungu huketi mahali penye sifa na Mungu anapenda sifa. anapenda sana sifa. msifu na mshukuru kwa kila ulicho nacho na sasa hapo u(chomekee na mahitaji mengine) tuache kumlaumu Mungu. hili ni kosa kubwa tunafanya. lawama kwa Mungu. tunasahau kuwa tunapolalamika kuwa mimi sijala na familia yangu. kuna mwingine chakula anapata lakini hawezi kula. au analishwa kwa mirija hata ladha ya chakula hapati. au akila chote kinatoka. 
Ukiwa unapiga Story na Mungu acha Majungu, fitna ,Umbea na Uchonganishi. usimpe hizo story.
acha majungu na umbea… “ooo Mungu mbona flan umemsaidia, mbona flan anakula bata, mbona flan anatutesa hapa mtaani” hayo ni majungu. wewe omba au piga story zako achana za kuwafitinisha watu na Mungu. hiyo ni kazi ya shetani asilimia 100. kama unataka kupiga story za watu wengine kwa Mungu basi ziwe njema kuwa unamsifu kwa kuwa amemtumia flan kuwasaidia watu flan.lakini siyo kumwaribia mwenzio kuwa anapata utajiri wakati ye mlevi mzinzi au si mwema kama wewe…hizo siyo issues za kupiga story na Mungu. acha majungu fanya yako.
tumshukuru Mungu huyu baba yetu na sisi wana wake kwa sifa na utukufu. watu wanashangaa mtu akisema yeye ni mwana wa Mungu. kwa nini?kama shetani ana watoto wake na kwa nini Mungu asiwe na watoto wake? 
Unaweza mshawishi Mungu akufanyie jambo mpaka akakubali kulifanya.
unapokaa na Mungu kupiga story hebu jifunze kumshawishi. mshawishi afanye jambo lako ikiwa ni jema. yeaah yu can do that. sometime Mungu anakuwa hakukuweka kwenye ratiba flan. lakini kama utamshawishi anaweza akakufanyia Upendeleo. na Mungu anatoa Upendelea kutokana na Ushawishi wako na Kazi zako.Si kweli kuwa Mungu hana Upendeleo. anao. kwa nini unadhani si wote wamelazwa muda huu? unadhani kwa nini wewe umekula?kwa nini wewe mzima? unadhani ni sababu wewe ni mwema sana au unastahili kuliko aliyepata ajali jana na juzi au mgonjwa wa kusubiri kufa?
well..upendeleo wake hauhusian na mali au uzuri wa nje. kila jambo Mungu hufanya kwa kusudi au huruhusu litokee kwa makusudi
Mungu anapenda sana Sifa hasa akiwa anapiga story na Shetani
Usidhani Mungu na Shetani hawaongei. wanaongea. tena huwa sometime wanatambiana sana. Mungu anatamba kwa shetani kwa watu wake wema wanaotenda mema. rejea habari ya Ayubu katika kitabu cha Ayubu 1:7 Shetani akiwa katika mizunguko yake ya kila siku ya kutafuta watu wa kuwapoteza akapita sehemu Mungu akamwona akamwuuliza “unatoka wapi?” naye akajibu kuwa anatoka katika kuzunguka zunguka huko na kule. Kwa majidai kabisa Mungu akamwuliza Shetani “unamwona mtumishi wangu Ayubu? maana hakuna aliye mkamilifu kama yeye…..”
Mungu anajivunia Ayubu. unadhan wewe ikitokea Shetani amekutana na Mungu nani atajivuna kwa mwenzie?anyway, wadau msisite ku kaa na kupiga story na Mungu na ukiwa katika story usipige story za hovyo hovyo. jiheshimu na umheshimu. muombe kwa unyenyekevu na kujishusha na pia uwe na subira usiforce mambo.ndo hapo unasema Mapenzi yako yatimizwe.
Jifunze kudeka kwa Mungu. anapenda sana kudekeza aisee…tena utaenjoy sana.
sometime unaweza hata deka kwa Mungu. unajua anapenda sana kudekeza. hivi umewah kuwaangalia ndege wa angani? walivyo wazuri na wenye kupendeza. hivi uliona wapi mashamba wanayolima? uliona wapi wakifuma nguo au manyoya wanayotumia? anyway. wewe ni bora kuliko wale ndege. wewe una thaman kuliko wale ndege. MUNGU NI BABA YAKO. Issues nyingine mweleze tu reality a juhudi zako then mwambie umemwachia yeye. unataka mke…mwambie wewe umeshajipanga na upo tayari sasa naye akupige tafu maana wewe huwezi jichagulia mke. mke mwema anatoka kwa Mungu.basi akupe mtoto mkali mwema anayekufaa. basi. unaachana na hiyo issue unasubiri. kama una vifungu vya kumkamatia kwenye biblia hebu mtajie. mkumbushe mwoneshe unajua unachoomba. sometime wewe dai mambo yako kupitia tu maandiko yake then mwachie. au kama kuna mazuri unatenda mkumbushe wala si dhambi
Haya, njooni, tusemezane, asema Bwana.Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji, zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi, kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga;maana kinywa cha Bwana kimenena haya
(Isaya 1: 18-19)
Mungu ni Rafiki, Mungu hataki aogopewe, Mungu anapenda wana wake… Sisi ni wana wa Mungu na kama sisi ni wana wa Mungu basi sisi ni Miungu. “ninyi ni miungu” katika Zaburi 82: 6 na Yohana 10:34?”

from Blogger http://ift.tt/2s3CwMH
via IFTTT