TzTown Tv: CHUMBA CHA UPASUAJI CHAJENGWA UWEMBA NI FARAJA KWA WAKAZI

WAKINAMAMA wakazi wa kata ya Uwemba halmashauri ya Mji Njombe wamesema kuwa wamekuwa wakifuata Mbali huduma za Upasuaji na wengine kujifungulia Njiani wakati wafufuata huduma hiyo huku baadhi yao wakesema kunavifo vimekuwa vikitokea wakati wakifuata huduma hiyo katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe Kibena.
Wakazi hao wamekuwa wakifuata huduma za upasuaji katika Hospitali Teule ya Rufaa ya mkoa wa Njombe Kibena kutokanana Kituo cha afya ambacho wamekuwa wakikitegemea kuto kuwa na huduma za upasuaji.
Serikali inafungua chuma cha upasuaji ambacho kimejengwa na kanika Katoriki kwenye kituo cha afya cha Mtakatifu Anna Uwemba.
Kaimu Askofu wa Kanisa Katoliki wakati wa Ufunguzi anasema kuwa kazi ya kanisa ni kuhakikisha watu wanakuwa salama kiafya kiroho na kimwili.
Wakazi hawa wanasema kuwa baada ya kufunguliwa kwa kituo hiki sasa wanauhakika wa kujifungua salaama wakifika Hospitalini hapo.


CHUMBA CHA UPASUAJI CHAJENGWA UWEMBA NI FARAJA KWA WAKAZI………………

from Blogger http://ift.tt/2s5xoZu
via IFTTT