Kimenukaa Cuf..Maalim Seif Ampasua Prof Lipumba..Atoa Kauli Hii Nzito kwa Hasira ..!!!

VITA vya maneno vimezidi kushika kasi ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) na sasa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ameibuka na kumtaka aliyekuwa mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, amwache kwa kuwa hana uwezo wa kumfukuza kazi.
Kadhalika, amesema kama kweli Profesa Lipumba anadhani yeye ni mwenyekiti halali, afike makao makuu ya CUF kisiwani Unguja ili kufanya kazi badala ya kukubali aendelee kutumika.
Hivi karibuni Profesa Lipumba alitangaza kumfukuza kazi, Maalim Seif na kumteua Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Tanzania bara, Magdalena Sakaya, kuwa kaimu Katibu Mkuu.
Akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho katika kisiwa kidogo cha Tumbatu Mvuvini, Maalim Seif alisema anamshangaa Profesa Lipumba kwa madai kwamba yeye ameshindwa kazi kwa kuwa haendi kazini katika ofisi za chama zilikozo Buguruni, Dar es Salaam.
“Eti nimeshindwa kazi akidai kuwa siendi ofisi kuu ya CUF Buguruni. Mbona yeye haji makao makuu ya CUF Mtendeni. Lipumba hana mamlaka ya kuniondoa nafasi yangu ya ukatibu mkuu,” alisema.
Alisema tangu Agosti, 2015, Lipumba hajawahi kukanyaga makao makuu ya CUF Mtendeni na kwamba hata kama angekuwa Mwenyekiti halali wa chama, alipaswa kumwita na kumhoji kwa nini haendi ofisi kuu za chama Buguruni kuliko kuchukua madaraka ya kutangaza kuwa amemtimua.
Maalim Seif pia alikemea siasa za chuki na uhasama zilizotawala kisiwani humo kati ya CCM na CUF na kusema zimesababisha mapigano na hujuma ikiwamo kuchomeana nyumba kutokana na itikadi za vyama.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alisema Profesa Lipumba ametumika na amefanya kazi kubwa ya kukihujumu chama huku akiungwa mkono na baadhi ya wanachama.
Mazrui pia alimwomba Rais John Magufuli kumtimua Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kwa madai kuwa ni miongoni mwa watendaji wabovu wa serikali.
Alisema utendaji mbovu wa Jaji Mutungi umesababisha mtafaruku mkubwa na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF.
“Rais Magufuli anatumbua watendaji ambao si waadilifu, lakini Msajili amemwacha kwani anapaswa kutumbuliwa kwa sababu ameivuruga nchi,” alisema.
Alisema Msajili huyo amempa uhalali Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF, wakati alijiuzulu kabla ya uchaguzi mkuu na sasa amekuwa akikihujumu chama.

from Blogger http://ift.tt/2n0Zhms
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2oN5oY9
via IFTTT

Related Posts

Fahamu Tabia za Wanawake Wanaopenda Sana Pesa Mapenzi 1. Huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima. Wanawake wengi wapendao pesa huwa na tamaa ya mambo yasiyo ya lazima, mambo ambayo hayagusi maisha moja kwa moja. Hata nilipokuwa chuo wanawake wengi waliokuwa wanapenda pesa Sana walikuwa na tamaa za kusikitisha ambazo zilipofusha fahamu zao. Unakuta mwanamke anaomba laki tano kwaajili tuu ya kununua Simu nyingine kubwa wakati akiwa bado na simu mpya. Katika maisha ni bora uingie jehanam kuliko kukutana na mwanamke mpenda pesa kwani utateseka Sana kwa ajili yake na bado hata ona msaada wako. Sio rahisi kujenga familia bora na mwanamke mpenda pesa. 2. Wengi hutoka familia masikini. Wanawake wengi Kama sio wote ambao hupenda pesa kuliko utu wao hutoka familia kame Sana. Ukame wa kiuchumi mpaka kiakili. Wengi wao huweza kutoa hata rushwa ya ngono ili tuu wapate pesa wasijue miili yao inathamani zaidi ya zile karatasi. Mtu ni masikini unandoto za kuwa na mwanaume mwenye pesa nani alikuambia wenye pesa wanataka masikini. Umasikini wako usikufanye ujidharau au mtu akudharau. Lipo kundi dogo la wanawake wanaojitahidi kutetea thamani ya jinsia yao lakini wengi wao ni wakuonewa huruma tuu. 3. Wengi wao hawana elimu ya kutosha. Mwanamke aliesoma akaelimika hawezi hangaika na pesa ya mtu. Ndio maana wanawake wachache huhangaika kwajili ya kujitegemea na sio kumtegemea mwanaume. Wanawake wengi wenye elimu na vipato vizuri huwezi msikie akiongelea pesa Kama kigezo muhimu kwa mwanaume anayemuhitaji awe mume wake. 4. Ni wavivu na wasio na mawazo. Wanawake wote wanaopenda pesa ni wavivu kupita kiasi. Uvivu wao umeanzia akilini kiasi kwamba hawana mawazo ya maendelo. Utakuta mwanamke anawaza mambo mepesi kabisa Kama urembo, nguo, mtoko, n.k. Wanawake wapenda pesa ni hatari kwa ustawi wa familia. Huwezi kuwa na familia kubwa ukiingia katika bahari ya viumbe hawa. 5. Hawana shukrani wala uvumilivu. Wanawake wapenda pesa huwezi msikia akikushukuru zaidi ya kujichekesha tuu na kubinua makalio. Kwa mfano amekuomba milioni moja then ukampa laki tano basi utamsikia akisema sasa hii nitafanyia nini, au niongezee tena mume wangu huku akikushika kifua au ndevu. Wanawake wenye hekima hushukuru mpaka mwanaume anasikia aibu. Suala la uvumilivu halipo kwa hawa wanawake. Shida ikitokea ukishindwa kuitatua kwa wakati huo basi hesabu umeliwa. Yaani kwao kukusaliti ni jambo lisilo na mashaka.