Kamati ya Makamu wa Rais Yatembelea vyanzo vya maji

KAMATI ya mazingira ya kusimamia mto Ruaha na vyanzo vyake iliyoundwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suruhu hivi karibuni imeanza kupita maeneo mbalimbali yenye vyanzo vya maji vya mto huo Nyanda za juu Kusini ili kubaini changamoto zinazo sababisha mto huo kukosa maji. 
Kamato hiyo ikiwa mkoani Njombe kwa siku mili siku yake ya kwanza imepita katika halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe na kuzungumza na wakazi wa wilaya hiyo na baadhi ya watumishi na kutermbelea vyanzo viwili vya maji kati ya vingi vya mto Ruaha.
Kamati ikiwa hapa Wanging’ombe watumishi na baadhi ya viongozi wa kada mbalimbali wanaeleza changamoto za kupambana na uharibifu wa mazingira huku madhara yake nayo yakitajwa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo kwa mkoa wa Njombe ambaye pia ni katibu tawala wa mkoa Jackson Saitabahu anasema kuwa jukumu la kulinda maji ni la pande mbili.
Hata hivyo Tanesco, Sagcot ni wadau ambao wanaingia katika kamati hiyo ambapo Tanesco inasema umeme unaotokana na maji ni Bei nafuu zaidi ukifuatiwa na ule wa Gesi.

from Blogger http://ift.tt/2oeyRyu
via IFTTT


Related Posts