HUYU NDIYE RAIS WA KWANZA WA AFRIKA KUKUTANA NA RAIS DONALD TRUMP

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi yupo, Washington, D.C nchini Marekani ambapo anatarajia kukutana na Rais wa Marekani, Donald Trump na kufanya naye mazungumzo.
Rais Abdel Fattah al-Sisi atakuwa kiongozi wa kwanza kutoka barani Afrika kukutana na Rais Trump. Lakini pia, alikuwa ndiye kiongozi wa kwanza wa Afrika kuzungumza na kumpongeza Trump baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika Novemba 8, mwaka jana.
Masuala ya mgogoro kati ya Palestine na Israel yanatarajiwa kutawala sehemu kubwa ya mazungumzo yao, lakini pia masuala ya ugaidi duniani wakiegemea zaidi kupambana na kundi la kigaidi la Dola la Kiislamu (ISIS).
Viongozi hawa walikutana Septemba mwaka jana jijini New York wakati Rais Sisi alipokuwa nchini humo kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa (UN).

from Blogger http://ift.tt/2otjm54
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nADRZA
via IFTTT

from WordPress http://ift.tt/2nwom4e
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nT4WtG
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2nwGE5a
via IFTTT

Related Posts