Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24 Machi, 2017 amewaapisha Mawaziri wawili, Katibu Mkuu Ikulu, Mabalozi wanne na Kamishna wa Tume ya Mahakama, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Walioapishwa ni Mhe. Dkt. Harrison George Mwakyembe aliyeapishwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi aliyeapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, na Bw. Alphayo Kidata aliyeapishwa kuwa Katibu Mkuu – Ikulu.
Wengine ni Mhe. Sylvester Mabumba aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Dkt. Abdallah Possi aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mhe. Job Masima aliyeapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Israel na Mhe. Jaji Stella Esther Mugasha aliyeapishwa kuwa Kamishna wa Tume ya Mahakama.
Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi hao, Mhe. Rais Magufuli amewataka kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa na kwa kutanguliza maslahi ya Taifa na pia amewasihi kutobabaishwa na kauli ama vitendo vyovyote vya kuwavunja moyo.
Mhe. Rais Magufuli pia amewasihi waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kutanguliza maslahi ya Taifa badala ya kutoa kipaumbele katika masuala ya migogoro na mambo mengine yasiyo na manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Nchi yetu huko nje ina sifa kubwa sana, juzi tu hapa amekuja Rais wa Benki ya Dunia na amekubali kutupatia Shilingi Trilioni 1.74 na pia Benki ya Dunia ipo katika mchakato wa kutupatia fedha zingine Shilingi Trilioni 2.8 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, haya ndio mambo muhimu ya kuandika lakini hebu angalia siku iliyofuata jinsi magazeti yalivyoandika” amehoji Mhe. Rais Magufuli.
Aidha, amewaonya wamiliki wa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikiandika habari za uchochezi na amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kuhakikisha vyombo vya habari vinafanya kazi kwa kufuata sheria na havitumiwi kuvuruga nchi.
Kabla ya kuwaapisha viongozi hao, Mhe. Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 6 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi hao ni Balozi wa Cyprus hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Muscat – Oman Mhe. Andreas Panayiotou, Balozi wa Bangladesh hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi – Kenya Mhe. Meja Jenerali Abdul Kalam Mohammad Humayun Kabir na Balozi wa Nepal hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Pretoria – Afrika Kusini Mhe. Amrit Bahaur Rai.
Wengine ni Balozi wa Ecuador hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Addis Ababa – Ethiopia, Balozi wa New Zealand hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Pretoria – Afrika Kusini na Balozi wa Jamhuri ya Kongo mwenye makazi yake Mjini Kigali – Rwanda Mhe. Michael Gerrard Burrel.
Katika mazungumzo yake na Mabalozi hao Mhe. Rais Magufuli amewapongeza kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano na nchi hizo, huku akitilia mkazo ushirikiano katika masuala ya uwekezaji, biashara na kubadilishana uzoefu katika uzalishaji mali hususani kilimo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waapishwa baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam Machi 24, 2017 Waapieshwa hao ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, huku Waziri mpya wa Sheria na katiba Profesa palamagamba kabudi akiwa pembeni baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam Machi 24, 2017
Waapishwa wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Kutoka kushoto ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Profesa Palamagamba kabudi baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Cyprus hapa nchini Andreas Panayiotou ambaye makazi yake yapo Muscat, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Bangladesh hapa nchini Maj. Gen. Abdul Kalam Mohammad Humayun Kabir mwenye makazi yake Nairobi, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Bangladesh hapa nchini Maj. Gen. Abdul Kalam Mohammad Humayun Kabir mwenye makazi yake Nairobi mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Nepal hapa nchini Amrit Bahadur Rai ambaye makazi yake yapo Pretoria Afrika Kusini mara baada ya kupokea hati zake za utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ecuador hapa nchini Benys Toscano Amores ambaye makazi yake yapo Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Ecuador hapa nchini Benys Toscano Amores ambaye makazi yake yapo Addis Ababa nchini Ethiopia mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa New Zealand hapa nchini Michael Gerrard Burrel ambaye makazi yake yapo Pretoria nchini Afrika Kusini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Congo Brazaville hapa nchini Guy Nestor Itoua ambaye makazi yake yapo Kigali nchini Rwanda.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Machi, 2017
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
from Blogger http://ift.tt/2nMfzPS
via IFTTT