Je unatazama video au kufanya kazi ambayo hutaki watu wachungulie na kujua unafanya nini? Basi kampuni ya HP imekuja na laptop inayokulinda dhidi ya wachunguliaji.
HP (Hewlett-Packard) wamekuja na laptop mbili tofauti ambazo vioo (display) vyake vinauwezo wa kupunguza mwanga kwa hadi asilimia 95 kama mtu anaangalia laptop hizo kutoka upande flani – kushoto au kulia.
Kila utazamaji unavyokuwa wa pembeni ndio kioo kinazidi kuwa cheusi. Uwezo huu unakuja na laptop za HP EliteBook 1040 na EliteBook 840
Teknolojia hiyo walioipa jina la Sure View inasemekana itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watumiaji wanaopenda usiri wa vitu wanavyofanya kwenye kompyuta (laptop) zao. Kuna laptop mbili zitakazokuja na teknolojia hii, laptop za inchi 14. Na Sure View itaweza kuwezeshwa kwa kubosha F12 katika keyboard.
Tafiti zinaonesha udukuzi wa kuchungulia kwa pembeni au nyuma kuona kompyuta za watu mara nyingi zinafanikisha lengo la mchunguliaji – na pia ni njia rahisi zaidi kuliko udukuzi wa kimtandao.
Tazama video Mtoto amvua kofia
Papa Francis
Papa Francis
from Blogger http://ift.tt/2nqr9wo
via IFTTT